loader
Picha

Kanyasu ataka Makumbusho kujiendesha kibiashara

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amelitaka Shirika la Makumbusho ya Taifa kujiendesha kibiashara. Pia alitaka shirika hilo kujenga makumbusho ya marais katika Mkoa wa Dodoma, ujenzi wa makumbusho ya tembo, nyumba za jamii za watanzania katika Kijiji cha Makumbusho.

Mengine ni uendelezwaji wa vituo vya malikale, ujenzi wa jengo la kuhifadhia magari yaliyopo Makumbusho na hata kurejesha mabaki ya mijusi aina ya Dinosaur yaliyopo Ujerumani. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika Makumbusho ya Nyumba ya Utamaduni, Kanyasu alisema ni muhimu taasisi ya makumbusho kubadilika na kufikiri zaidi kibiashara.

“Mjitangaze, mna mambo makubwa mnayoyafanya yaliyomo ndani ya taasisi hii lakini yanaweza yakawa hayafahamiki ipasavyo,” alisema Kanyasu na kuwataka kuwa wabunifu zaidi na kuweka suala la utalii kwa ukaribu zaidi. Alisema kwa kubadilika wanaweza kuwa shirika linalotoa gawio kwa serikali kama ilivyo taasisi nyingine, huku ikikamilisha na kutekeleza maagizo yaliyoelekezwa kwao.

Kuhusu maagizo, Kanyasu alisema namna bora ni kuanzisha utekelezwaji wa maagizo hayo ili kujulikana walikofikia na walikokwama, ingawaje wanajulikana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kifedha. “Hivi aliyetoa agizo la kujenga makumbusho ya marais, akifika atauliza maandalizi yamefikia wapi? Mmekwama wapi...fanyeni kwa awamu, kama hamjaanza basi inawezekana kuonekana haipo kabisa,” alisema Kanyasu huku akiongeza kuwa wizara imekuwa ikisikitika kuona kadiri siku zinavyokwenda shirika hilo ambalo ni kubwa inazidi kulialia kila siku.

Alisema wanahitaji kuona wanakuwa wabunifu, kuwa imara zaidi, kufikiria kibiashara zaidi huku wakitoa elimu lakini ikiwa kibiashara zaidi. Awali Kaimu Mkurugenzi katika Makumbusho, Mawazo Jamvi alisema mikakati mikubwa ya shirika hilo ni kuongeza idadi ya watalii jambo ambalo ni la msingi kwao. Kuhusu maagizo ya ujenzi wa makumbusho mbalimbali, alisema yapo yaliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii na hata Naibu Waziri lakini pia na Waziri Mkuu kuhusu kushirikiana na wakuu wa mikoa kujenga nyumba za jamii za Watanzania.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi