loader
Picha

TAMWA yapata mkurugenzi mpya

CHAMA  cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimemtangaza Rose Rueben kuwa mkurugenzi mtendaji wake mpya kujaza nafasi inayoachwa wazi na Edda Sanga, anayemaliza nafasi yake. 

Mkurugenzi huyo mpya amekabidhiwa ofisi rasmi leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Tamwa zilizopo Sinza Mori, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama mbalimbali wa chama hicho. 
Dk. Rose Ruben  aliwahi kufanya kazi  Radio Tanzania Dar es Salaam, sasa TBC Taifa, Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF), kabla ya kuamua kuachana na shirika hilo na kufanya shughuli zake binafsi huku akiendeleza harakati za kumkomboa mwanamke na watoto.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa wadhifa wa kuongoza taasisi hiyo,Rose alisema: “Nitaendeleza harakati za kumkomboa mwanamke na watoto, kupinga ukatili wa kijinsia, kufanya kazi kwa kufuata katiba, kanuni na sheria za nchi ili tusitoke nje ya sheria za  nchi yetu, naomba tushirikiane kuhakikisha Tamwa inasonga mbele, tuchape kazi kwa maendeleo ya Tamwa na jamii ya watanzania wanaotuzunguka, hapa kazi tu.”

Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo, Tamwa inatekeleza mradi wa kupinga ukatili kwa watoto na wanawake katika wilaya saba lakini chini ya uongozi wake atahakikisha mradi huo unatekelezwa Tanzania nzima.

“Natamani mradi huu ufike Tanzania nzima,  ili nchi iweze kuendelea ni lazima kuwepo na wanawake wenye afya njema ya kimwili na kiakili, na hilo litawezekana endapo watatendewa haki.

“Hata nyinyi wanaume ili muweze kufanya kazi zenu vizuri na kuishi vizuri ni lazima watendeeni  mema wanawake hususani wake zenu, wachumba zenu, hao ni sawa na dada na mama zenu, natamani kuona vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake vinamalizika, Tanzania bila ukatili wa wanawake na watoto inawezekana," amesisitiza.

Naye Edda Sanga analiyemaliza muda wake ametoa rai kwa waandishi wa habari wachanga kujiongeza hususani katika kujiendeleza kielimu ili kuendana na kasi ya maendeleo duniani.
 

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi