loader
Picha

Rais Shein awaachia huru wafungwa

KATIKA kusherehekea miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewaachia huru wanafunzi 12 wa vyuo vya mafunzo waliopo visiwa vya Pemba na Unguja.

Vyuo vya mafunzo ni sawa na magereza Tanzania Bara na wanaohudumu adhabu zao (wafungwa) huitwa wanafunzi. Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Mohamed Yahya Mzee, Rais aliwaachia huru wanafunzi hao kwa kutumia Kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kifungu hicho 59 (a), (b), (c) na (d) kinaeleza kuwa Rais anaweza kutoa msamaha bila masharti au kwa masharti kwa mtu yeyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote; Kutoa uahirisho ama wa muda au wa moja kwa moja katika kutekeleza adhabu yoyote, iliyotolewa na Mahakama kwa mtu huyo kuhusiana na kosa alilotenda; Kubadili adhabu aliyopewa mtu kutokana na kosa lolote na kuifanya iwe ndogo zaidi; Kumsamehe kabisa au kwa kiasi fulani mtu yeyote aliyepewa adhabu kwa kosa lolote au adhabu ya utaifishaji iliyotolewa na serikali dhidi yake.

Alisema kwa mujibu wa maamuzi ya Rais na kwa nguvu aliyopewa na Katiba, wanafunzi hao 12 vifungo vyao vimefutwa kuanzia Januari 11 mwaka huu. Aliwataja walioachiwa huru kutoka Unguja kuwa ni Mustak Mustafa Bashiri, Ramadhani Abubakar Jabu, Bakari Hamisi Juma, Maulid Heri Suleiman, Othmani Ramadhani Shija, Faiz Juma Faiz na Ali Haji Ali.

Wengine ni Suleiman Ali Suleiman, Ali Omary Ali, Ibrahim Mbaruk Omar, Mohamed Othman Ali na Mbarouk Ali Mbarouk, wote wakiwa ni wa vyuo vya mafunzo Pemba. Kwa mujibu wa maelezo wanafunzi wote wanaotumikia adhabu za mauaji, wizi wa kutumia nguvu, wizi wa mali za umma, wadhalilishaji wanawake na watoto, dawa za kulevya hawahusiki na msamaha huo.

Kilele cha miaka 55 ya mapinduzi ni leo, ambapo kutakuwa na shamrashamra mbalimbali katika Uwanja wa Gombani mjini hapa, ambapo Rais wa Zanzibar, Dk Shein anatarajiwa kuhutubia taifa. Maandalizi katika mji wa Chakechake ni makubwa na ya utulivu na bendera na vitambaa vya rangi ya njano, nyeusi, bluu na kijani vipo katika maeneo mengi. Vijiwe vipo tulivu na kahawa inaendelea kunywewa bila tashwishi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe, Chakechake

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi