loader
Picha

Chuki iliyokuwepo Pemba sasa haipo

JOTO kubwa la kisiasa kisiwani Pemba lililokuwepo katika miaka ya 1990, limepoa na wananchi wameanza kutambua umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani na kupambana na maisha.

Hali hiyo inatokana na wananchi wa makundi mbalimbali, kuona fursa za ushirikiano kuwa bora zaidi kuliko husuda na chuki zilizokuwapo kipindi hicho. “Kubaguana kwa wazi kulikokuwepo wakati huo hakupo, lakini siasa zipo lakini za chuki na ugomvi zimepungua sana, “ alisema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed wakati wa mahojiano na gazeti hili.

Alisema uchaguzi wa mwaka 1995, ulileta mihemko mingi na hali ya sintofahamu, lakini kwa sasa hali imetulia. “Hata leo nimetoka shambani na kutembea kwa miguu. Kila mtu sasa anaweza kutembea kifua mbele bila shaka, chuki imeondoka imebaki siasa,”alisema. Aboud ambaye mwaka 1995 alikuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, alisema anazikumbuka vyema siku hizo, ambazo maisha Pemba yalikuwa na shaka kubwa hata miongoni mwa ndugu. Alisema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za serikali za kuendelea kutuliza munkari, kwa kupeleka maendeleo zaidi na kutumia fursa zilizopo katika kufikisha maendeleo kwa wananchi wake.

“Watu wanaona maendeleo, wanajua maendeleo hayana chama, tunapeleka maendeleo wanaona ndio siri ya kutulia, japo mioyoni mwao siasa zitakuwepo,” alisema Aboud. Alisema wameleta mabadiliko katika siasa na kuruhusu vyama vingi, hivyo siasa zitaendelea kuwepo, lakini chuki kwa kizazi cha sasa zinaisha. “Watu wengi wa sasa hawakuona mapinduzi, lakini faida ya mapinduzi inaendelea kuonekana, watu kufanyakazi na kupata maendeleo kutokana na kazi zao,” alisema Aboud. Alisema pamoja na fursa za maisha kuwa chachu ya uhusiano mwema, lakini ziara za viongozi zimekuwa zikibadili maisha na fikira za wengi katika kuheshimu umuhimu wa kazi na maisha katika kisiwa hicho.

“Tuna nafasi kubwa zaidi ya kusahau mabaya na kukumbuka mema na nia ya kuwapo kwa mapinduzi, kwani haya ndio matunda ya mapinduzi ukombozi kutoka katika utumwa na ukoloni, kutuletea maendeleo ya kiafya,” alisema. Kisiwa cha Pemba chenye mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini na wilaya nne, ni kisiwa chenye ukijani, hali inayoruhusu utalii wa kimaumbile na kilimo.

JESHI la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kumteka ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe, Chakechake

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi