loader
Picha

Waziri wa Viwanda aipa somo FCC

TUME ya Haki ya Ushindani nchini (FCC) imetakiwa kutotumia kigezo cha mapungufu ya nguvu za kisheria, kama kigezo cha kutowashughulikia wahujumu wa uchumi wanaogushi bidhaa za nje na kuziuza hapa nchini.

Mwito huo umetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda jana wakati akizungumza na wafanyakazi wa FCC kwenye makao makuu ya tume hiyo. Alisema kumekuwa na matukio mengi yanayofanywa na walanguzi, ambapo wakikamatwa na askari, maofisa wa tume hiyo wakifika hushindwa kuchukua hatua kwa kigezo cha kutokuwa na nguvu za kisheria.

Aliwataka kutambua kuwa mlanguzi au mtu anayepakia bidhaa za nje kwa kutumia vifungashio vya ndani ili zionekane kuwa zimetengenezwa hapa nchini ni sawa na mhujumu uchumi. “Ndio ninatambua kuwa mnazo changamoto za kisheria katika kushughulikia masuala mbalimbali ila kinachotaka hiyo isiwe kigezo cha kushindwa kuchukua hatua, zipo sheria mama zinazoweza kutumika kuwashughulikia watu wanaopakia bidhaa za nje kwenye mifuko ya hapa nchini ili zionekana zimetengenezwa hapa,” alisema.

Aliongeza kuwa huo ni uhujumu uchumi na kwa nini wasishughulikiwe, lakini pia aliahidi kuwa wizara imejipanga kusaidia uharakishwaji wa mapendekezo yao ya sheria ili yakamilike kwa wakati na wawe na nguvu ya kufanya mengi zaidi. Pia Waziri Kakunda aliitaka FFC kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kuandika andiko la pamoja litakalowawezesha kusaidiwa na China katika kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki tangia zikiwa China Alisema hatua hiyo itasaidia kuzuia uingizwaji wa bidhaa bandia na kumkinga mlaji dhidi ya bidhaa hizo huku akiwataka wafanyakazi wa tume hiyo kufanya kazi kwa uzalendo,uadilifuna uaminifu.

Aliahidi pia kusaidia kuimarishwa kwa muundo wa uundwaji wa tume hiyo ili kusaidia kuimarisha utendaji mzuri zaidi na kusaidia upatikanaji wa huduma bora zaidi. Mwenyekiti wa FCC, Humphrey Moshi akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri alibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabilia tume hiyo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa nguvu za kisheria za kuiwezesha tume hiyokufanya kazi.

Alisema pia kuwa tume hiyo inakabiliwa na changamoto ya muundo ambapo alishauri kuwa inatakiwa kupanuka kijiografia kwa kuwa na ofisi nchi nzima pamoja na wafanyakazi wengi na kuongeza kuwa mwishoni mwa mwezi huu FCC itahamia rasmi Dodoma ambapo imeanza ujenzi wa jengo lake jipya.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi