loader
Picha

Nditiye: ATCL acheni kufanya kazi kwa mazoea

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameiagiza menejimenti ya Shirika la Ndege Nchini (ATCL) kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa ofi sini.

Badala yake, ametaka watoke kusimamia mradi wa karakana ya ndege na shule ya marubani, uliogharimu zaidi ya Sh milioni 624 uliopo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kwani mkandarasi aliyepewa zabuni ya kukarabati karakana ile, hawezi kumaliza ndani ya wakati na hilo serikali halitalikubali. Mbali ya menejimenti kuamriwa hivyo, pia Bodi ya ATCL imeagizwa kufuatilia kwa karibu mradi huo, maana serikali haitakuwa tayari kuona mkandarasi anafanya kazi nje ya muda, kwani itabidi yeye ndio ailipe serikali.

Aliongeza kuwa zabuni yake imetolewa vipande vipande na huko ni kuiingizia hasara serikali bila ya sababu za msingi. Nditiye alitoa maagizo hayo juzi, alipotembelea karakana hiyo na jengo la kuweka rada ya ndege katika uwanja wa KIA akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira. Alisema hajaridhishwa na ukarabati wa karakana, ila ameridhika na ujenzi wa jengo la rada.

Alisema mkandarasi aliyepewa zabuni ya kukarabati karakana ya ATCL na shule ya marubani, ana muda wa wiki mbili tu kukabidhi kazi kwa mujibu wa mkataba. Lakini, alisema dalili ya kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ni ndoto na jambo baya zaidi hana msimamizi wa karibu kutoka ATCL .

Nditiye alisema pamoja na maelezo yake kuwa atakamilisha ndani ya wiki mbili kukarabati sakafu na paa, kazi iliyobaki ni kubwa na kibaya zaidi zabuni ya kuweka umeme hahusiki nayo na kuweka vipooza hewa pia sio kazi yake, hatua ambayo serikali itapata hasara, kwa jengo hilo kutangazwa zabuni yake vipande vipande.

Alisema Sh milioni 624 aliyolipwa mkandarasi ni fedha nyingi za walipa kodi wanyonge, hivyo ni lazima fedha hizo zionekane, kwa kazi inayolingana na thamani ya kazi yake na sio vinginevyo. Kutokana na hali hiyo, aliitaka menejimenti ya ATCL kuamka na kwenda eneo la karakana kusimamia kazi na kuacha tabia ya kukaa ofisini kusubiri ripoti kutoka kwa mkandarasi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi