loader
Picha

‘Sare za jeshi’ 1,947 zanaswa kambi za wakimbizi Kigoma

NGUO za mitumba zipatazo 1,947 zinazofanana na sare za jeshi, zimekamatwa katika kambi za wakimbizi za Nduta Wilaya ya Kibondo na Mtendeli Wilaya ya Kakonko, zikigawanya kwa wakimbizi hao.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Kigoma, Samson Anga amesema kuwa sare hizo za jeshi, zilikamatwa Desemba 31 mwaka jana asubuhi. Alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma. Akieleza kuhusu sare hizo, alisema kuwa katika sare hizo zilizokamatwa, 1,325 zilikamatwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta na sare nyingine 1,622 zilikamatwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli zikiwa zinagawanywa na viongozi wa jumuia ya wakimbizi kambini hapo.

Anga ambaye ni Mkuu wa Wilaya Kigoma, alisema kuwa shirika moja linalotoa huduma za wakimbizi kwenye makambi hayo linahusika na uingizaji wa sare hizo kwenye makambi ya wakimbizi. Alisema kuwa wapo watu waliokamatwa kutokana na tukio hilo. Hakutaja watu hao kwa sasa kwa kusema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea. Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa makambi ya wakimbizi, ni marufuku kwa wakimbizi kuvaa nguo au sare zozote zinazofanana na sare za kijeshi.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi