loader
Picha

Mapinduzi ni fahari ya kila Mzanzibari

LEO wananchi wa Zanzibar sambamba na wenzao wa Bara wanaungana kuadhimisha miaka 55 ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar ya mwaka 1964.

Sherehe za Mapinduzi huadhimishwa Januari 12 kila mwaka, kwa lengo la kutunza historia hii adhimu na pia kukifahamisha kizazi cha sasa Zanzibar ilipotoka, ilipo sasa na inakokwenda.

Sherehe za leo pia zimekuwa zikitumika mara kwa mara kwa ajili ya ufunguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kabla ya Mapinduzi hayo, Wazanzibari walitawaliwa na mataifa mbalimbali wakiwamo Waarabu, Wajerumani na Waingereza. Watu weusi waliwekwa katika daraja la chini ambapo walidharauliwa, kunyanyaswa na kukandamizwa wakiwa ndani ya nchi yao wenyewe.

Baada ya kupigania uhuru kwa muda mrefu bila kupewa, Waingereza waliamua kutoa uhuru kwa Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar. Kitendo hicho kilisababisha Wazanzibari wengi kuendelea kukosa uhuru kamili kwa kuwa uongozi wa Kisultani uliendelea kuwaweka waafrika katika daraja la chini. Mpango wa Mapinduzi ulifanikiwa siku kama ya leo mwaka 1964 na hivyo kuung’oa utawala wa Kisultani na kisha wananchi walio wengi, wakashika hatamu ya kuongoza dola, chini ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume.

Mapinduzi ya Zanzibar ni tukio muhimu ambalo wananchi wanapaswa kulikumbuka na kujivunia kwani kuanzia mwaka 1964 Wazanzibari wamekuwa huru katika nchi yao, wakijipangia mambo yao wenyewe kwa ajili ya maendeleo yao. Haki zote ambazo wananchi wazalendo walistahiki kuzipata ikiwemo elimu, matibabu na matumizi ya ardhi kwa kilimo na makazi ambavyo walinyimwa na utawala dhalimu wa Kisultani sasa wanazipata kutokana na mapinduzi hayo.

Kwa lugha rahisi, ni mapinduzi hayo ndiyo yaliyomrejeshea haki mwafrika, haki ambayo aliyo nayo hadi leo ikiwemo kuunda chama cha siasa na kujiendeleza kadri anavyoweza. Ni mapinduzi yaliyokuwa pia chanzo cha Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuzaliwa Tanzania. Ni vigumu mtu kupata picha hali ingelikuwaje kuhusu muungano kama Sultani angeendelea kutawala visiwa vya Zanzibar.

Pamoja na umuhimu wa mapinduzi haya yaliyomrejeshea Mzanzibari uhuru wake alionao leo pamoja na haki yake kama mkazi halali wa visiwa hivi kuna Wazanzibari walio katika kambi ya upinzani wamekua wakisusa kushiiki katika maadhimisho haya. Huko nyuma pia, kabla ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, Wapinzani walikuwa na kawaida ya kukisusa pia sherehe za kuadhimisha mapinduzi haya matukufu. Lakini kitu ambacho kimekuwa kikiwashangaza wengi ni Wapinzani kuchukia hata kutamka neno “Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” au kwa kufupi “SMZ”.

Hatua hiyo kwa kweli ni sawa na kusema wapinzani wanachukizwa na mapinduzi! Hii imekuwa ikileta wasiwasi pia kwamba siku upinzani ukichukua uongozi wa dola, upo uwezekano wa kufuta sherehe za mapinduzi moja kwa moja. Lakini kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha Wakulima (AFP_, Said Soud amekuwa akisema kwamba sherehe za mapinduzi ni za kitaifa na hazipaswi kuhusishwa na itikadi ya vyama vya siasa. Soud ambaye kwa sasa ni Waziri asiye na Wizara Maalumu aliwahi kukaririwa akisema kwamba sherehe hizo ni utambulisho wa wananchi wa Zanzibar walivyojikomboa kutoka kwenye utawala wa Kisultani kwa hivyo zinatakiwa kuenziwa na kutunzwa na sio kubezwa au kususwa kama wanavyofanya wanasiasa wengine.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi