loader
Picha

Kampuni 4 zaingia mikataba ubanguaji korosho

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga ameshuhudia hafl a ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani ili bidhaa hiyo iweze kubanguliwa hapa nchini hatimaye kuongeza wigo wa ajira kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania, Dk Hussein Mansoorndiye ametia saini kwa niaba ya serikali na kampuni nne zimesaini mikataba ya awali kuanza kazi hiyo ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, pamoja na Micronix- Newala.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa hafla hiyo, Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imepitia vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuanza kuingia makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya ubanguaji wa korosho.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya kubangua jumla ya tani 7500 kwa hatua za awali ambapo kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd ina uwezo wa kubangua tani 2000 kwa mwaka ambayo imesaini mkataba wa tani 1500. Nyingine ni Kampuni ya Micronix ya mjini Mtwara tani 2400 kwa mwaka ambayo imeingia mkataba wa tani 1200, Kampuni ya Korosho Afrika ya Mjini Tunduru mkaoni Ruvuma tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua tani 2400 na kampuni ya Micronix ya wilayani Newala yenye tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua tani 2400.

Alisema kazi hiyo ya ubanguaji tayari ilikuwa imeshaanza kupitia Shirika la Kushughulikia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) ambalo tayari limeajiri wafanyakazi 160. Waziri Hasunga alisema kuwa shirika hilo pamoja na majukumu mengine lakini lilikuwa na kazi mbili ambazo ni kuhakikisha wanatengeneza vipuli na mashine mbalimbali ambazo zimeharibika pamoja na kuhamasisha wabanguaji wadogo wadogo na kuwasajili.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Mtwara

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi