loader
Picha

Yusufali, wenzake 3 wakabiliwa na mashitaka 640

MFANYABIASHARA, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake watatu wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka 640, ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 16.

Awali, Yusufali na wenzake wawili, Alloyscious Mandago na Isaac Kasanga, walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka 39 ikiwemo kusababisha hasara ya Sh bilioni 2.9 katika kesi namba 1 ya mwaka 2019. Katika kesi nyingine, Yusufali na mfanyabiashara, Arifal Paliwala walisomewa mashitaka 601 ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Sh 14,987,707,044.58.

Kesi hizo zilisomwa kwa mahakimu wawili tofauti, ambao ni Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. Akisoma hati ya mashitaka mbele Hakimu Mmbando, Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole alidai mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao ni kugushi, kutoa nyaraka za uongo, kufanya biashara bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mashitaka 18 ya utakatishaji.

Akisoma mashitaka hayo, alidai kuwa kati ya Machi 2, 2010 na Aprili 26, 2016 katika maeneo tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam, washitakiwa hao walikula njama kwa kughushi, kukwepa kulipa kodi na kutakatisha. Katika mashitaka ya pili, mshitakiwa Kasaga anadaiwa kuwa kati ya Mei 9,2016 katika ofisi za Wakala wa Usajili (Brela) zilizopo Manispaa ya Ilala, aliwasilisha nyaraka za uongo yenye fomu namba 128 ya Mei 2,2016 akionesha kuwa Machi 4,2012 wakurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited ni Mohamed Yusufali, Isack Kassanga na Maria Barnett.

Ngole alidai katika mashitaka mengine ya utakatishaji fedha kuwa kati ya Machi 4,2011 na Aprili 13, 2016 katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Yusufali akiwa mmiliki na Mkurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited, walijihusisha na muamala wa kiasi cha Sh 2,967,959,554 wakijua fedha hizo zinatokana na zao la fedha haramu. Baada yakusomewa mashitaka hayo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo. Hata hivyo, Wakili Ngole alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika, hivyo wanaandaa maelezo ya mashahidi kwa ajili ya shauri kwenda Mahakama Kuu.

Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Wakati huohuo, mfanyabiashara Yusufali na Paliwala walisomewa mashitaka 601 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mashauri. Akisoma mashitaka hayo jana, Wakili Ngole alidai kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kati ya Januari 26 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam, walikwepa kodi na kughushi nyaraka mbalimbali na kuisababishia serikali hasara ya Sh 14,987,707,044.58. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Wakili Ngole alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilik,a hivyo wanaandaa taarifa za mashahidi kwaajili yakwenda Mahakama Kuu. Hakimu Mashauri aliwataka washitakiwa kutojibu chochote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi