loader
Picha

Simba: Yes We Can

SIMBA leo inashuka katika dimba la Taifa, Dar es Salaam kuivaa JS Souara ya Algeria kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika ikiwa na matumaini ya ushindi mbele ya mashabiki wake.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kocha wa Simba Patrick Aussems na kocha wa JS Souara, Neghiz Nabil kila mmoja alijigamba kuibuka na ushindi na kusifu kikosi cha mpinzani wake. Aussems alisema katika kikosi chake atamkosa Erasto Nyoni, ambaye aliumia goti la kulia kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, lakini akasema nafasi yake itazibwa na wachezaji wengine kwani Simba ina wachezaji wa kutosha mashabiki wasiwe na hofu.

“Tunaiheshimu sana JS Souara maana wanatoka kwenye nchi yenye ligi nzuri Afrika na wanashika nafasi ya tano katika ligi ya kwao, tutamkosa Erasto Nyoni ambaye amekuwa katika kiwango bora katika michezo aliyocheza lakini wapo watu wa kuziba nafasi yake,” alisema Aussems Tunawaomba Watanzania waje kuishangilia Simba ili ipate nafasi ya kuchukua ubingwa wa Afrika kama walivyofanya katika mchezo dhidi ya Nkana Rangers,” aliongeza Naye kocha wa JS Souara Nabil alishukuru kwa maandalizi mazuri waliyopata na kusema Simba ni timu bora zaidi yao ila wanatamani kushinda mchezo wa leo.

“Nashukuru tulifika jana (juzi) na tulipata mapokezi mazuri, tunaiheshimu Simba lakini ninatamani kushinda mchezo wa kesho (leo) ili kujiweka katika nafasi nzuri katika kundi letu,” alisema Nabil Pia alisema Thomas Ulimwengu kulingana na rekodi zake ni mchezo mzuri lakini kwa sasa anahitaji mazoezi sana ili arudi katika kiwango chake na katika mchezo huo atamkosa kipa wake mmoja.

Simba ambayo ipo kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo DRC na JS Saoura ya Algeria inashuka katika dimba la Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kuitoa Nkana Rangers ya Zambia kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo ina kibarua cha kuhakikisha Al Ahly ambayo ilicheza fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Esperance Tunis ya Tunisia msimu uliopita inazifunga pamoja na AS Vita Club ambayo ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewaomba Watanzania kuungana naye kuishangilia Simba ili ishinde mchezo huo kwasababu hao ndio wawakilishi wa nchi waliosalia. “Nawaomba Watanzania tuoneshe uzalendo kwa Simba, tuishangilie kwa nguvu kuanzia dakika ya kwanza hadi dakika 90 ili ishinde kwa sababu ndio wawakilishi pekee waliosalia,” alisema Dk Mwakyembe. Mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk Tulia Akson, ambaye atawaongoza maelfu ya Watanzania kuishangilia Simba. Msemaji wa Simba, Haji Manara ameibuka na kauli mbiu inayosema, `Simba Yes We Can’, kuelekea mchezo huo wa leo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi