loader
Picha

Uchaguzi Yanga kizungumti, wasimamishwa

UCHAGUZI wa Yanga ambao ulikuwa ufanyike kesho Jumapili katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa Polisi, Osyterbay, Dar es Salaam umesitishwa baada ya wanachama kuweka pingamizi mahakamani.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela alisema wameamua kuahirisha uchaguzi huo baada ya kuwepo pingamizi mahakamani mikoa mbalimbali.

“Ndugu waandishi ratiba yetu ya uchaguzi wa Yanga ni Jumapili, sasa wakati tupo kwenye kikao tukapata taarifa kuwa kuna baadhi ya wanachama wa Yanga wamefungua kesi za kusimamisha uchaguzi hapa Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na Morogoro na sehemu nyingine,” “Sasa sisi kama kamati hatutaki kugongana na mhimili wa mahakama, kwa sababu tumesikia kuna sehemu nyingine wameanza kusikiliza mashauri hivyo tumeamua kusimamisha uchaguzi usifanyike Jumapili hadi tupate courty order maana kesi nyingine zimeanza kusikilizwa leo na Jumatatu tutawaita ili tuwaambie nini kinaendelea,” aliongeza Mchungahela.

Pia alisema wale waliokuwa wanaendelea na kampeni wasimame na hata ule mdahalo, ambao ulikuwa ufanyike jana Azam TV haukufanyika kwa sababu hiyo. Jumla ya wagombea 16 wanawania nafasi mbalimbali, ambapo nafasi ya Uenyekiti wapo ni Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga, makamu Mwenyekiti ni Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota .

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi