loader
Picha

Yanga warejea katika ligi

MENEJA wa timu ya Yanga, Nadir Haruob Canavaro amesema kuwa wanarudi nyumbani kwa ajili ya kwenda kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara na lengo lao kubwa ni kuweza kurejesha ubingwa wao ambao hivi sasa unashikiliwa na Simba.

Canavaro aliyaeleza hayo hivi karibuni baada ya timu yao kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwenye hatua ya makundi na kusema kuwa pamoja na kutolewa kwao, lakini vijana wake wamecheza mchezo mzuri. Aidha, alisema kuwa kutolewa kwao katika mashindano hayo mapema ni jumla ya matokeo ya mchezo, hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo ni ya wazi na kila timu inayokuja inakuwa imekuja kwa ajili ya kushindana.

Alisema kuwa mwaka jana na mwaka huu hawakuweza kufanya vizuri, ambapo mwaka jana walitolewa kwenye nusu fainali na mwaka huu hatua ya makundi. Alifahamisha kwamba katika mwaka huu, wamekuja na vijana ambao aliwasifia kwa kuwa wameonesha kiwango kizuri, licha ya kutokuwa na uzoefu wa kutosha. “Hivi sasa tunarudi kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa sababu ligi inaanza na wenzetu wengine wanaendelea kucheza kama, ambavyo mmesikia juzi matokeo ya ajabu Prison imeweza kumfunga Mtibwa Sugar na sisi tuna malengo yetu kurejesha ubingwa ambao uko kwa Simba, “alisema.

Alisema kuwa mechi yao wanatarajia kucheza Januari 16, mwaka huu, na timu ya Mwadui FC na wamejipanga kushinda ili kuzidi kuchanja mbuga katika msimamo wa ligi hiyo. Aidha, alishukuru kwamba vijana hao wameonesha viwango vizuri na kupata uzoefu wa kutosha na mwalimu ameona kupitia TV na kikubwa wanachokishukuru ni kwamba wamemaliza mashindano hayo bila kupata majeruhi yoyote. Yanga ilipangwa katika Kundi B na timu za Azam, Malindi, Jamhuri na KVZ na kutolewa katika hatua ya makundi licha ya kushinda 3-1 mchezo wa mwisho dhidi ya Jamhuri.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi