loader
Picha

Azam yatangulia fainali Mapinduzi

MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi Azam FC jana walitinga fainali ya mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kwenye Uwanja wa Amaan hapa.

Kwa ushindi huo, Azam FC sasa inamsubiri mshindi wa mchezo jana usiku kati ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba dhidi ya Malindi kwenye uwanja huo huo, kucheza fainali itakayopigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba kesho.

Azam tangu mwanzo wa mchezo huo walionekana wakipania kuibuka na ushindi baada ya kulishambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara na kubahatika kupata bao katika dakika ya tisa na Aggrey Moris. Wakati mabao mengi ya Azam ambao kama wakilitwaa taji hilo litakuwa lao kabisa baada ya kulitwaa mara mbili mfululizo, yalifungwa na Salum Aboubakar `Sure Boy’ katika dakika ya 64 na Obbrey Chirwa katika dakika ya 81.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi