loader
Picha

RC akerwa Moshi kupoteza ukinara wa usafi nchini

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imeelezea kukerwa kwake na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kupoteza hadhi yake ya kuwa kinara wa usafi miongoni mwa manispaa nchini kote kwa miaka 10 mfululizo.

Katika hatua nyingine, serikali imemtaka Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya kuacha kuchanganya siasa na masuala ya utendaji, kwani suala la usafi wa mazingira linahusisha afya na halihusu siasa. Mkuu wa Mkoa, Anna Mghwira alisema hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Soko la Mbuyuni na kushuhudia uchafu ukiwa umelundikana na mpangilio usioridhisha wa wafanyabishara wadogo.

Katika ziara hiyo, mkuu wa mkoa alisema hali iliyopo sasa imechangiwa na kutotekelezwa wajibu kwa ofisi ya mkurugenzi wa manispaa hiyo, meya na watendaji wengine wakiwamo wa mitaa. “Sijaridhishwa na hali ya usafi katika manispaa na mpangilio wa wafanyabiashara katika masoko, sielewi hili jambo linakwama wapi wakati tulishatoa maelekezo muda mrefu uliopita...nataka ofisi ya mkurugenzi kunipa maelezo yanayojitosheleza,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alisema anashangazwa na taarifa za baadhi ya wafanyabiashara kwamba wameruhusiwa kupanga bidhaa barabarani na meya wa manispaa hiyo. “Siwezi kuvumilia wanasiasa wanaotukwamisha katika shughuli za maendeleo kwa kauli zao za kisiasa... maendeleo na mazingira havina siasa, hii ni faida kwa wananchi wote bila kujali vyama vyao,” alisema.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi