loader
Picha

Utegemezi Zanzibar wapungua kwa asilimia 2.2

Hali ya utegemezi visiwani Zanzibar imepungua hadi 5.1% kwa mwaka 2018/19 ikilinganishwa na 7.3% ya mwaka 2017/18.

Haya yamesemwa mapema leo, Jumamosi, na Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein alipoongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dr Shein ameeleza kuwa mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na jitihada za serikali kukuza uchumi ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukusanyaji mapato.

“Kutokana na jitihada za serikali kuimarisha uchumi, ukusanyaji wa mapato uliofanywa na taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) umeongezeka hadi shilingi bil 688.7/- kwa mwaka 2017/18 kutoka bil 528/- za mwaka 2016/17,” alisema.

Tofauti na hilo, Dr Shein ameeleza kuwa moja ya sekta zilinazoendelea kushamiri kwa kasi ni ya nishati, ambapo hadi kufikia Desemba 2018 vijiji 2694 kati ya 3259 vimefikiwa na umeme katika visiwa vya Unguja na Pemba.

“Mafanikio haya ni 83%, na lengo letu ni vijiji vyote kuwa vimefikiwa na nishati ya umeme kati ya mwaka 2020/22,” aliongeza.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi