loader
Picha

Hongera Zanzibar kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi

WAZANZIBARI wameadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi adhimu ya Januari 12, 1964, ambayo yaliwapa uhuru kutoka kwa Sultani.

Sherehe hiyo iliongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na ilifanyika Kiwanja cha Gombani, Pemba.

Tunaungana na Watanzania wote kutoa pongezi kwa Wazanzibari kwa kuadhimisha siku ya uhuru wao na kuwataka wazidi kuudumisha.

Katika kuadhimisha siku hiyo, tumefurahishwa zaidi na habari kuwa kutokana na juhudi kubwa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika uimarishaji uchumi, ukusanyaji mapato umekua.

Rais Dk Shein aliwaeleza wananchi waliofurika kwenye sherehe hizo na kufuatilia matangazo ya televisheni na redio, mwaka 2017/18 SMZ ilikusanya Sh bilioni 688/7 ikilinganishwa na Sh bilioni 521.8 zilizokusanywa mwaka 2016/17.

Kupaa kwa makusanyo hayo ni ushahidi tosha wa mafanikio makubwa ambayo SMZ imepata, tangu Zanzibar ipate uhuru kiasi cha kuboresha huduma za jamii kwa kiwango kikubwa zaidi.

Ni kutokana na ushahidi huo tunawiwa kutoa pongezi kwa Wazanzibari wote na Rais Shein kwa mafanikio makubwa ambayo wamepata.

Mafanikio hayo yanaashiria kuwa Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatekeleza vyema dhana nzima ya kujitegemea kwa kusimamia vizuri uchumi.

Kwamba maadhimisho hayo, yamefanyika Pemba ni ushahidi wa wazi wa kurejea kwa umoja na mshikamano kati ya wananchi huko.

Ni vyema basi umoja huo, udumishwe kwa maslahi ya Wazanzibari wote na Tanzania kwa jumla, kwani amani ikosekana, inaathiri wote.

Ni matarajio yetu maendeleo makubwa ambayo yanaendelea kufanywa na SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatazidi kuwa chachu ya Wazanzibar kushikamana zaidi.

Miaka hii 55 inatosha kuwa kielelezo kwa watu wote, ambao bado wanaimezea mate Zanzibar, kuiacha iendelee kustawi kama Taifa lililo huru.

Na kwa kikazi kipya, miaka hiyo iwakumbushe kule wazee wao walikotoka na kuwajengea ujasiri wa kutumikia Taifa lao kwa uaminifu.

Wakifanya hivyo, watajihakikishia maisha bora zaidi, wakiwa na uhakika kuwa wako huru, hivyo kutumia zaidi muda wao kujenga uchumi imara.

MKUTANO wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi