loader
Dstv Habarileo  Mobile
Hongera Serikali kugeukia soko la utalii China

Hongera Serikali kugeukia soko la utalii China

KWA miaka mingi serikali imekuwa ikijitahidi kunadi vivutio vyake vya utalii katika sehemu mbalimbali duniani, hasa Marekani na mataifa mengi ya bara la Ulaya.

Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro, Selous, Rubondo, Mlima Kilimanjaro, Ruaha na Sadani.

Pia, malikale, maporomoko ya maji na Zanzibar ambako kuna fukwe murua.

Serikali imekuwa ikinadi vivutio hivyo, kwa sababu kwanza vinaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni, ambapo huingiza Dola za Marekani bilioni 2.3, sawa na Sh trilioni 5.04 kwa mwaka.

Pili, vivutio hivyo mchango mkubwa katika ajira, ambapo hutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya milioni 1.5 wanaofanya kazi mbalimbali, mfano kutoa usafiri wa ndani kwa watalii, kuongoza watalii na kuuza bidhaa kwa watalii kama vyakula, vinywaji, vinyago, nguo na zawadi.

Lakini, katika siku za karibuni, serikali imeanza kuelekeza jitihada kubwa katika bara la Asia, hasa taifa la China. Tunapongeza jitihada hizo zinazofanywa na serikali, hasa ukichukulia ukweli kwamba China ndilo taifa lenye watu wengi zaidi duniani.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana mwaka 2010, China ilikuwa na watu bilioni 1.4 mwaka huo. Nchi iliyoifuatia China kwa idadi ya watu ni India watu bilioni 1.3 na Marekani ilikuwa ya tatu, kwa kuwa na watu milioni 322.

Nafasi ya saba ilishikwa ni Nigeria, ambayo ilikuwa na watu takribani milioni 190. Kwa bara la Afrika, Tanzania inashika nafasi ya 5, kwa kuwa na watu milioni 55 na imezidiwa na nchi za Nigeria, Ethiopia, Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yenye watu takribani milioni 80.

Ni wazi kuwa kuwepo kwa idadi hiyo kubwa ya watu nchini China, ni fursa kubwa na ya kipekee kwa Tanzania, kwa sababu endapo nchi itafanikiwa kushawishi Wachina wengi kuja kutembelea, taifa litaongeza fedha nyingi zaidi za kigeni na pia litaongeza masoko mengi zaidi ya mazao na bidhaa zake mbalimbali.

Tumevutiwa mno na kauli ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyesema kuwa Tanzania inajipanga kuvutia watalii, kwa kugeukia uwekezaji katika hoteli zenye hadhi ya kimataifa na pia kuhakikisha inapokea watalii wengi, wakiwemo kutoka China.

Aidha, tunapongeza ziara maalum ya kuutangaza utalii wa Tanzania nchini China, iliyofanywa na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) na wadau wengine muhimu. Wakiwa China, maofisa hao walitembelea majimbo ya Shanghai, Guangzhou, Hong Kong, Chengdu na Beijing.

Kote huko walikuwa wakinadi kwa nguvu vivutio vya utalii. Kutokana na ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TTB, Thomas Mihayo anasema wanatarajia kupata watalii 10,000 zaidi mwaka huu.

Mwaka 2017, Tanzania ilipokea zaidi ya watalii 30,000 kutoka China. Kwa mujibu wa Mihayo, safari za ndege ya ATCL kati ya Dar es Salaam na Guangzhou nchini China kupitia Bangkok, Thailand na Mumbai, India, zinatarajiwa kuleta matunda mazuri kwa utalii wa Tanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/404b3cca8c6c2d939140b127488e4152.jpg

KWA mara ya kwanza leo dunia inaadhimisha ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi