loader
Picha

ATCL kusafirisha minofu ya samaki

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ipo katika mipango ya kusafirisha minofu ya samaki na nyama kutoka jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam kisha kusafirishwa nje ya nchi.

Akizungumza katika ziara yake ya siku moja mkoani Mwanza, Kamwelwe amesema wafanyabiashara wengi wa Mwanza wamekuwa wakisafirisha minofu ya samaki kupitia viwanja vya ndege vya Nairobi, Kenya na Entebbe, Uganda, jambo linaloonesha mizigo hiyo inatoka nchi za jirani wakati ni bidhaa za Tanzania.

Kamwelwe alisema safari hizo za kupeleka minofu hiyo nje ya nchi itasaidia serikali kupata mapato pamoja na ajira kwa vijana watakaokuwa wameajiriwa na viwanda vya uchakataji wa minofu ya samaki.

Waziri Kamwelwe alisema kupitia ziara yake hiyo ya siku moja, amegundua kwamba viwanda vya samaki mkoani Mwanza vina uwezo mkubwa wa kuzalisha minofu ya samaki tani 200 kwa siku.

Alisema amezungumza na wadau wa viwanda vya samaki na wamefurahishwa na juhudi za Rais John Magufuli kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria ili samaki waweze kuzaliana zaidi na zaidi.

ATCL ina ndege nane, Bombardier tatu, Airbus mbili na Dreamliner moja zilizonunuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano na mbili za Rais zilizotolewa kwa ATCL hivi karibuni ambazo zinafanya safari zake katika miji mbalimbali nchini na hivi karibuni zitaanza safari za kwenda nje ya nchi na mikoa mingine.

Tayari zimeanza kusafirisha nyama ya mbuzi kutoka Mwanza kwenda nje ya nchi kupitia Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Magese Mlai alisema uzalishaji wa minofu ya samaki Mwanza, umeongezeka na sekta yao ipo katika mikakati ya kuhakikisha inafanya uvuvi unakuwa endelevu ili kuweza kuipatia nchi mapato ya fedha za kigeni.

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi