loader
Picha

Watumishi kuhamishwa kuongeza mapato sokoni

MKUU wa Wilaya ya Tabora, Kitwala Komanya ameagiza mabadiliko ya watumishi wanaosimamia soko kuu kwa lengo kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Komanya alisema baadhi ya watumishi hao ndio wamekuwa chanzo cha kuwafanya wafanyabiashara wakwepe ulipaji mapato na wagome kulipa kwa sababu ya baadhi kuwa na maslahi ndani ya soko hilo.

Amesema hayo jana wakati wa kikao cha kupitia mapendekezo ya bajeti cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Tabora (DCC) cha Manispaa ya Tabora baada ya mjumbe kulalamikia upotevu wa mapato ya serikali.

Alisema wafanyakazi katika soko hilo hawatoshi kwa sababu hawaisaidii manispaa kukusanya mapato, na wamegeuka kama madalali wa wafanyabiashara na kusababisha ukusanyaji mdogo wa mapato.

Komanya amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa kuwaondoa na kuweka watumishi wazalendo ambao watasimamia vema soko hilo kwa maendeleo ya Manispaa ya Tabora na wakazi wake.

Alisema alipokutana na wafanyabiashara wa soko hilo kujua kero zao, watumishi hao walishindwa kumpa ushirikiano na kusababisha kutumia muda mwingi kusubiri ili apate mkutano wa wafanyabiashara hao.

DC Komanya pia ameagiza uongozi wa manispaa kuhakikisha unaendesha ukaguzi katika nyumba za kulala wageni ili kubaini wamiliki wake ambao wamekuwa hawaandikishi watu wanaolala katika nyumba zao katika vitabu vya wageni kwa ajili kukwepa kulipa kodi stahili.

Amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti watu wanaotoa taarifa potofu walipe kiwango kidogo cha ushuru.

Komanya amesema, ni vema manispaa ikaweka kila nyumba ya kulala wageni vitabu vyenye nembo yake kujiridhisha kama kinachoandikwa na kukusanywa kinalingana na idadi ya wageni waliolala katika nyumba hiyo.

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika ...

foto
Mwandishi: Tiganya Vincent, Tabora

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi