loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanamuziki Oliver Mtukudzi afariki dunia

Mwanamuziki maarufu wa nchini Zimbabwe, Oliver Mtukudzi, 66, amefariki dunia leo Jumatano, January 23, kwenye moja ya zahanati jijini Harare nchini, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Familia yake imethibitisha taarifa za kifo chake kupitia mtandao wa Twitter lakini ugonjwa uliopelekea kifo chake haujawekwa wazi.

Mpaka kifo chake Oliver alikuwa na jumla ya albamu za muziki 66.

Amefanya 'show' mbalimbali kwenye majukwaa mbalimbali Afrika na duniani kote.

Japokuwa anafahamika kwa nyimbo nyingi, vibao vyake vya Todii na Neria vinatajwa kuwa ndiyo vibao vilivyomuongezea umaarufu zaidi duniani.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi