loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kenya kufumua sekta ya umma

SERIKALI ya Kenya inatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya umma mwakani, kwa kuhakikisha watumishi wake wanahudumia wananchi ipasavyo, ikiwemo kusitisha kuajiri wafanyakazi ajira za kudumu, bali kuwapa mikataba ya miaka mitano.

Aidha, katika maboresho hayo wafanyakazi wa umma katika serikali kuu na zile za mitaa, watakuwa na fursa sawa katika haki zote.

Msaidizi wa Waziri katika Wizara ya Huduma za Umma,Vijana na Masuala ya Jinsia nchini Kenya, Rachel Shebesh, akizungumza katika kipindi cha Jukwaa la KTN katika Kituo cha Luninga cha KTN, alisema maboresho hayo, yanatarajiwa kukamilika Machi au April mwakani.

Alisema ili kufikia malengo hayo, wameanzisha kampeni ya huduma kwa wananchi kuhakikisha raia wake anapata huduma inayofaa kwa kuwa wanalipa kodi.

Shebes alisema kampeni hiyo ni juhudi za Umoja wa Afrika (AU), kuifanya nchi hiyo kuwa ya majaribio katika kuboresha utendaji kati kwa sekta ya umma na kuondoa vitendo vya rushwa na ufisadi, ikiwemo kuondoa umasikini kwa wananchi wan chi hiyo hatimaye kuwa mfano kwa nchi nyingine.

Alibainisha kuwa AU wameanza na Kenya kwa kuwasimamia na baadaye kufuatia katika nchi nyingine na tayari wameanzisha vituo maalum vya kutoa huduma 52 vinavyotoa huduma 88 za kwa kuwahudumia asilimia 95 ya wananchi wake.

Alisema kwa sasa wamejipanga kupeleka vituo hivyo vijijini (Mashinani), kwa kujikita kuwa na vituo vya kuwahudumia wanawake na vijana, kwa kuhakikisha maafisa wake wanafanya kazi kwa kuwajibika kwa kuwa na huduma halisi kwa sekta zote.

Waziri alieleza kuwa katika kampeni hiyo, inashirikisha raia wake kwa kutoa taarifa kwa maafisa wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na watendaji wake, wanavyofanya vema katika utoaji huduma mbalimbali, kama vyeti vya kuzaliwa, hati za kusafiria na nyinginezo.

Alisema katika vituo vya kutoa huduma wanahudumia watu 50,000 kwa siku, lakini bado kuna maafisa wa serikali walioko ofisini na kutoa huduma, ambao ndiyo wanawasiwasi wa kuendeleza utoaji huduma isisvyostahili.

“Maboresho haya yatakayofanyika tunatarajia kukamilisha Machi au Aprili mwakani ikiwemo wafanyakazi wote wa serikali kuu na zile za mitaa kuwa na fursa sawa katika kupandishwa vyeo, kutoa ajira mpya, kustaafu kwa waliofanya kazi muda mrefu na kuingiza utaalamu

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi