loader
Picha

Mkulima auawa akizuia ng'ombe wasile mazao

MKAZI wa Kijiji cha Makole aliyetambulika kwa jina moja la Ally ameuawa kwa kukatwa mapanga.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe amethibitisha kutokea mauaji hayo yaliyofanyika kijiji cha Makole, Kata ya Kwalukonge wilayani Korogwe.

Kamanda Bukombe alisema mauaji hayo yalitokea baada ya mfugaji, Paulo Marko (24) kuingiza mifugo yake katika shamba la Ally, na katika mabishano, ndipo Marko aliamua kumkata mapanga hadi kufikwa na umauti.

“Ni kweli kumetokea mauaji katika Kijiji cha Makole, Kata ya Kwalukonge wilayani Korogwe ambapo mfugaji Paulo Marko amemuua bwana Ally wakati akitetea mazao yake,” alisema.

Aliongeza, “mfugaji aliingiza ng’ombe wake kwenye shamba la mkulima akaanza kula mazao na mkulima huyo alipomwambia aondoe ng’ombe wake, katika mabishano ya muda mrefu ndipo ikafikia hali hiyo ya mauaji.”

Diwani wa Kata ya Kwalukonge, Luka Rogan alisema baada ya mfugaji huyo kufanya mauaji alikimbia, lakini wafugaji wenzake walitoa ushirikiano, na walimkamata na kumkabidhi kwa Jeshi la Polisi wilayani Korogwe.

Alifafanua kuwa tatizo la migogoro ya ardhi katika kata hiyo ni ya muda mrefu na imekjuwa ni chanzo cha mauaji.

“Kwa kweli katika Kata ya Kwalukonge migogoro ya ardhi ndio chanzo kikubwa na tayari suala hili nimelifikisha kwenye vikao vya baraza la madiwani na uongozi wa wilaya,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Kwame Daftari amesema changomoto hiyo ya ardhi kwa wakulima na wafugaji inatafutiwa ufumbuzi.

Hivi karibuni, serikali kupitia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula alitangaza kufutwa kwa hati za mashamba tisa ya mkonge kati ya 14 yaliyokuwa yakimilikiwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) wilayani Korogwe kwa kushindwa kuyaendeleza ili yatumiwe na wananchi wa maeneo hayo kwa malisho

IDARA ya Habari (MAELEZO) imewataka wadau wa habari kufanya utafiti ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Korogwe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi