loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ubora City wamtesa kocha Arsenal

UNAI Emery alionekana kukata tamaa kabisa kutokana na kiwango kilichooneshwa na Manchester City walipocheza dhidi ya Arsenal na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad.

Mabao matatu `hat-trick’ ya Sergio Aguero’, pamoja na ushindi wa Chelsea na Manchester United mwishoni mwa wiki, ina maana Arsenal sasa wako nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu, pointi tatu nje ya nne bora.

Ingawa Arsenal walikuwa katika mchezo wakati matokeo yakiwa 1-1 wakielekea mapumziko, Emery anafikiria kuwa Man City ilionesha kiwango chake bora zaidi ya dakika 90 na ingawa walistahili ushindi.

Alisema: “Walionesha ubora wao katika kipindi cha dakika 90 na zaidi. Dakika 45 za kwanza, tulikwenda vizuri na matokeo, tulizuia pamoja nakufanya mashambulizi ya kushtukiza, ….

“Lakini baada ya kufungwa 2-1, kwa kweli katika kipindi cha pili walionesha umwamba wao. Hatukuwa na nafasi kabisa kuingia katika boksi, na matokeo yako wazi kabisa.

“Tulitakiwa kucheza pamoja kwa upande wa kuzuia na kushambulia, lakini hatukuweza kupata matokeo tuliyoyataka. Lakini leo (juzi) nafikiri wameonesha tofauti kati ya Man City na sisi, na changamoto yetu sasa ni kufanya kazi na kujiimarisha zaidi.”

Arsenal walishindwa kabisa kupiga shuti katika kipindi cha pili, baada ya bao la dakika za mwisho la Aguero, ambalo lilidhihirisha kipigo kwa kikosi cha Emery. Lakini Emery anasema sasa ni muhimu kuwa watulivu wakati Arsenal wakijikuta wako mahali pagumu, wakigombea nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

“Nafikiri [City] walicheza katika ubora wao katika dakika zote 90, na kiwango chetu kilikuwa kibovu katika kipindi cha pili zaidi ya kipindi cha kwanza. “Tulitaka kuwa katika mchezo kwa kipindi chote, lakini kipindi cha pili na baada ya bao, akili zetu hazikuwa kabisa mchezoni.”

“Ninajiamini katika kazi yangu, hivyo sasa kinachotakiwa ni kuwa watulivu zaidi.”

OFISA Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore, anatarajia kuachiwa wadhifa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi