loader
Picha

Mbwa muaminifu, ana upendo, anateseka

KATIKA nchi zinazoendelea, watu wengi hawajui faida za ufugaji wa mbwa na siyo jambo geni kuona mbwa ananyanyasika kwa kutopewa matunzo yanayostahili.

Katika muswada wa kitabu kiitwacho Bustani ya Mbwa kilicho mbioni kutolewa, nimetaja ukosefu wa elimu na hamasa kuhusu umuhimu wa ufugaji wa mbwa, ndio chimbuko la masaibu yanayomkumba mnyama huyu ambaye amekuwa rafiki wa mwanadamu takribani miaka 15000 iliyopita.

Watu wanafanya kosa la kumchukulia mbwa kuwa mnyama wa kufokewa, kupigwa mawe na watoto, kutupiwa makombo na hata kufungiwa kwenye chumba kidogo chenye giza. Kimsingi, mbwa anataka urafiki wa dhati na wanadamu ili awatumikie, awape usalama, atende mema na kuepuka uovu.

Mbali na madhila anayokumbana nayo ya mtizamo hasi wa mwanadamu, bado mbwa ana matumaini kwamba siku moja urafiki kati yake na mwanadamu utakuwa mtamu.

Ndiyo maana pamoja na kufokewa, kupigwa, kukosa chakula, kukosa mahala pazuri pa kulala, bado mbwa anavumilia na kutii maelekezo bila kinyongo kwa bwana wake.

Wakati hayo yakijiri, jamii ya sasa inapata changamoto na inatumia mbinu mbalimbali zikiwamo za gharama kubwa ili kuimarisha ulinzi hususani wa nyumbani.

Katika uchunguzi kwa watu na maeneo mbalimbali kwa muda mrefu, imebainika kuwa, watu wanajaribu kuzungushia himaya zao kuta nene na mageti mazito, lakini wezi wanaruka kuta na kuiba vitu mbalimbali ndani ya himaya hizo kama vile nguo, viatu, kuchomoa vifaa vya magari, uvunjaji na vingine.

Imebainika kuwa licha ya kujemnga kuta hizo, pia watu wamejaribu kuajiri walinzi binadamu ili kuongezea ulinzi wa kuta na mageti, lakini walinzi wamekuwa wakiwasaliti waajiri wao, kutamani mali zao, kulala kwa siri, kuacha lindo, na kuomba udhuru wa mara kwa mara ukiwamo wa kuuguliwa au kufiwa sambamba na uvivu.

Haya, hayapo kwa mlinzi mbwa. Upungufu mwingine wa walinzi wanadamu ni pamoja na manung’uniko, madai ya mara kwa mara ya nyongeza ya mshahara, kudai likizo na mengine mengi, likiwamo la wengine kuwa na kinyongo dhidi ya mwajiri wao wapotofautiana hali inayochangia pia kuwapo kwa baadhi wanaofanya hujuma.

Laiti watu wangejua faida za mbwa, wasingesumbuka kama wanavyohangaika hivi sasa kwani mbwa ni mnyama mtatuzi wa changamoto nyingi za kiusalama kwani licha ya hayo, hata gharama za kumhudumia mlinzi mbwa ambaye ni mwaminifu zaidi maana hapokei rushwa wala kutoa siri, ni ndogo kuliko gharama za kumwajiri mlinzi mwanadamu.

Kutokana na watu kutokujua faida zake, mbwa ametelekezwa na kukumbwa na kila aina ya adha. Wakati mbwa ndiye suluhisho la ulinzi wa uhakika, wanadamu wameendelea kumpuuza na kubaki na changamoto hizo.

Ama kweli ni kichekesho; mwenye shida anamkataa mtatuzi, ambaye yuko tayari kumsaidia pasipo masharti, bila hila wala kutaka mshahara.

Watu kwa kutojua thamani ya mbwa, wengi wamewaacha wazurure mitaani katika hali ya ukiwa wakati wana uwezo mkubwa wa kulinda uhai na mali zao. Kimsingi, tatizo halipo kwa mbwa, bali lipo kwetu kwa watu kutojua umuhimu wa ushirika na mbwa.

Pamoja na adha zinazowakumba mbwa, upendo wao kwa wanadamu umeendelea kuwa wa dhati, wakivumilia mateso yote bila kuchoka, kuwa waaminifu wakati wote katika huduma ya ulinzi bila hila wala manung’uniko. Taasisi kama vile, Umoja wa Wadau wa Mbwa (TCA–Limited), TAWESO, Kila Kiumbe Hai, TSPCA, Animal Heaven zinapaswa kuendelea kufanya kampeni kubwa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu matumizi na ufugaji bora wa mbwa.

Aidha, ni wakati mwafaka sasa wa kuanza kutumia sheria ya Haki za Wanyama ya Mwaka 2010, ili kutia msukumo unaohitajika katika kampeni hii.

Mbwa yeyote ana faida hasa katika eneo la ulinzi na ambaye hajafundishwa kabisa, bado anaweza kutoa huduma za ulinzi kwa kiwango cha kuridhisha.

Huduma za ulinzi zitolewazo na mbwa Zipo aina mbili za huduma za ulinzi zitolewazo na mbwa yaani, mbwa mwangalizi na mbwa mlinzi. Mbwa mwangalizi analinda himaya bila kuwa na ujuzi na anabweka anapohisi au kuona watu au wanyama (kwa ajili ya kujihami).

Kwa kitendo hiki, hutuma ujumbe kwa bwana wake kuhusu uwepo wa tishio la kiusalama. Zipo faida za kuwa na mbwa mwangalizi, hasa hilo la kumtisha adui asisogelee himaya. Kwa kuwa mgeni hana taarifa za aina ya mbwa aliyepo, anaamini atakiona cha mtemakuni akivuka ‘mstari mwekundu’.

Muswada unasema: “Atahisi mwenye nyumba anaweza kuitikia kelele za mbwa, kiasi cha kumlazimisha achukue uelekeo mwingine kuepuka tafrani. Maswali haya yote yatamfanya mtu mwenye nia mbaya kughairi kuingia katika himaya na kufanya uhalifu.”

Hata hivyo, tatizo la mbwa mwangalizi ni kule kubweka pasipo kufanya tathmini ya tishio la kiusalama; anaweza kubweka kwa kishindo cha paka, ndege, wadudu au panya anayepita. Mwenye nyumba anaweza asijishughulishe wakati wa hatari akidhani ni kelele tupu za mbwa mwangalizi.

Aina nyingine, ni mbwa mlinzi, ambaye hutoa huduma akiwa na ujuzi wa kazi anayoifanya kwa kuwa amefundishwa au ana upeo wa juu wa uelewa katika fani hiyo.

Anaweza kusoma mazingira na kutambua uzito wa hatari iliyopo mbele yake, kubuni na kuchukua hatua mwafaka ikiwa ni pamoja na kubweka, kushambulia, kukamata na kutoa taarifa kwa mwenye

BANDARI za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na zinginezo ...

foto
Mwandishi: Dk Egyne Emmanuel

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi