loader
Picha

Hongera Vodacom, CCBRT kupambana na fistula

HABARI kwamba Taasisi ya Vodacom Tanzania Faundation kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT wametoa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye fi stula na kuwawezesha kufi ka hospitali ni habari za kufurahisha.

Tunasema ni za kufurahisha kwa kuwa wanawake hawa wanahitaji matibabu na wala sio kunyanyaswa au kunyanyapaliwa kutokana na hali zao, kama ilivyo kwa siku za sasa.

Fistula ambayo ni hali isiyokuwa ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka bila kuzuilika.

Kutokana na haja ya kuwarejesha wanawake wenye matatizo hayo katika hali ya kawaida, kitendo cha kuanzisha programu maalumu kwa kuwapatia matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa, ni cha kutia moyo.

Hali hiyo imekuwa ikiwaweka wanawake takribani 3,000 kila mwaka katika hali ya kutengwa na jamii ambayo kiukweli haijui sababu na pia wapi pa kupata matibabu, japo inaeleweka kabisa kwamba fistula inatibika.

Tunataka kusema kwamba kitendo cha matumizi ya MPesa kuwasaidia waathirika ili waweze kusafiri hadi CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu ni jambo la kufurahisha sana kwa kuwa wengi wa watu wenye tatizo hilo wanatoka katika familia maskini na hawana uwezo wa kusafiri.

Aidha kitendo hicho kitachochea wanawake wasio na uwezo kutafuta matibabu badala ya kuamini kwamba wamerogwa na kuachwa wakihangaika na kufadhaishwa na hali zao.

Kwa kuwawezesha wanawake wanaoishi na hali ya fistula kupata matibabu ya kiafya, wanakuwa wamewasaidia kiafya, kimwili na kisaikolojia kwa sababu wengi wao hutengwa na jamii zinazowazunguka kutokana na ugonjwa huo, pamoja na kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida na kujumuika kwenye jamii zao, CCBRT na Vodacom wamefanya maamuzi yenye tija kubwa kwa jamii.

Ingawa kumekuwepo na mafunzo kwa jamii kuhusu fistula kwa kuandaa semina mbalimbali ambazo zinaambatana na majadiliano ya changamoto mbali mbali zinazotokana na fistula, kitendo hiki cha sasa cha Vodacom kinatoa nuru zaidi katika mapambano haya.

Tunapenda kuamini kwamba kwa hatua hizo zitasaidia kukabiliana na tatizo la fistula hapa nchini ambalo Shirika la Afya duniani (WHO) linasema wanawake kama 3,000 hupata tatizo hilo kila mwaka hapa nchini.

Tunaamini mpango huo ulianzishwa na Vodacom Tanzania Foundation kama sehemu ya kuisaidia serikali kuboresha huduma za afya nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi utaamsha ari ya jamii kumsaidia mwanamke asitengewe kwa sababu ya fistula.

Kiukweli tunazipongeza juhudi za taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na CCBRT katika kukabiliana na matatizo ya kiafya yatokanayo na uzazi nchini na kuwasaidia wanawake kukabiliana na matatizo hayo na kuwa na taifa lenye siha njema na linalopamba wanawake.

MKUTANO wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi