loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kumekucha ligi ya mabingwa Ulaya

HATUA ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya inaanza Februari 12 na Shirikisho la Soka la Ulaya, UEFA, limekutana na klabu zote kuzungumzia hatua hiyo, na hasa matumizi ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR).

Teknolojia hiyo itatumika katika hatua hiyo ya mtoano ya mashindano hayo ili kuhakikisha mabao au adhabu zinatolewa kwa haki ili mshindi kupatikana kihalali.

Hatua hiyo ya mtoano ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, itaanza ndani ya wiki moja kuanzia sasa na VAR itatumika katika hatua hiyo itakayoanza Jumanne ya wiki ijayo.

UEFA iliwaalika wawakilishi wa klabu zote 16, ambazo zitashiriki msimu huu, ambapo zilikutana katika jiji la Ujerumani la Frankfurt ili kuelezewa kuhusu matumizi ya mfumo huo, ambao una lengo la kuwasaidia waamuzi kutoa maamuzi sahihi.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa teknolojia hiyo ya VAR kutumika katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, ambapo UEFA imekuwa ikiwapiga msasa waamuzi watakaochezesha mechi hizo ili kuufahamu zaidi.

Utumiaji wa teknolojia hiyo umeshuhudia maamuzi yaliyotolewa na mwamuzi kupitiwa upya kwa kuangalua picha za video, na hata kubadilishwa, endapo itaonekana yalitolewa kimakosa.

Makocha na wawakilishi kutoka klabu 16 zilizofuzu kwa hatua hiyo ya 16 bora walipata maelezo kutoka kwa kiongozi wa waamuzi wa UEFA, Roberto Rosetti, ambaye aliwashauri na kuwaelea jinsi VAR inavyotumika.

Timu inayosimamia VAR ni mwamuzi msaidizi pamoja na waendeshaji mashine hiyo ya video, watakuwepo katika kila uwanja ili kuwasaidia waamuzi na wasimamizi wa mechi ili kufikia maamuzi sahihi.

Rosetti alisema timu ya VAR itakuwa na kazi ya kuhakikisha maamuzi yanakuwa sahihi na makosa ya wazi yanarekebishwa.

Maamuzi ambayo yamekuwa yakibadilishwa ni yale ya penalti, magoli, kadi nyekundu ya moja kwa moja na kosa la bahati mbaya la kumpa adhabu mchezaji, ambaye sio aliyefanya tukio.

“Lilikuwa jambo muhimu kwetu kuzungumza moja kwa moja na wawakilishi wa klabu, “alisema Rosetti, “kuwaelezea jinsi watakavyotumia VAR katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, na sasa tunaanza kwa ajili ya waamuzi.”

“Tunashawishika kuwa VAR itakuwa na manufaa makubwa,” aliendelea Rosetti, “tunawapatia waamuzi msaada muhimu, na kuwawezesha kupunguza maamuzi yasiyo sahihi, ambayo yatakuwa mazuri kwa klabu, wachezaji, makocha, mashabiki na mashindano.”

Mbali na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, VAR msimu huu itatumika katika fainali ya Ligi ya Ulaya itakayofanyika Baku, fainali za Mataifa ya Ulaya huko Ureno Juni na yale ya fainali za Ulaya kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 huko Italia mwezi huo huo.

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka ...

foto
Mwandishi: NYON, Uswisi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi