loader
Picha

Shelisheli: Nchi ndogo zaidi Afrika

BARA la Afrika lina nchi 54 na nchi hizo zinatofautiana kwa ukubwa na idadi ya watu. Miongoni mwa nchi hizo iliyo ndogo zaidi inatajwa kuwa ni kisiwa cha Shelisheli ingawa kwa upande wa nchi kavu nchi ndogo zaidi ni Gambia.

Nchi hiyo ndogo zaidi ya Shelisheli inatajwa kuwa na kilomita za mraba 451 na kwa mujibu wa idadi ya watu hadi mwaka juzi ilikuwa ni 94,228. Idadi hiyo ni ndogo kuliko wakazi wa Wilaya ya Kigamboni hapa nchini ambayo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ilikuwa na wakazi 162,932 na ukubwa wake ni kilometa za mraba 416.

Shelisheli ambayo mji mkuu wake ni Victoria ilipata uhuru Juni 26 mwaka 1976 na ndiyo nchi inayoongoza barani Afrika kuwa na wakazi wachache. Wakazi wengi wa nchi hiyo ni masikini ingawa takwimu zinaonesha kuwa Pato la Taifa (GDP) la Shelisheli ni kubwa.

Umasikini huu unatokana na kwamba kuna tofauti kubwa ya kipato miongoni mwa raia wa nchi hiyo. Historia inaonesha kuwa kisiwa hicho awali hakukuwa na mtu anayeishi ila baadaye mabaharia kutoka Australia, Maldive na wafanyabiashara waarabu walihamia huko na ndiyo sababu wakazi wake kuwa mchanganyiko wa mataifa hayo na Ufaransa pia.

Hii ilibainika baada ya ugunduzi wa makaburi. Kisiwa hicho kilikuwa kikitumiwa na maharamia hadi mwaka 1756 kilipokuwa chini ya Ufaransa. Jina lake limetokana na Jean Moreau de S’echelles.

BANDARI za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na zinginezo ...

foto
Mwandishi: Maulid Ahmed

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi