loader
Picha

Tamasha ya Pasaka kufanyika Kijitonyama

KWA mara ya kwanza Tamasha la Pasaka litafanyika kwenye viwanja vya chuo cha Posta Kijitonyama jiji Dar es Salaaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama amesema tamasha hilo mwaka huu litafanyika Aprili 21 kwenye viwanja hivyo badala ya Uwanja wa Taifa, wilayani Temeke.

"Safari hii tamasha litafanyika chuo cha Posta, tumeangalia unafuu wa usafiri, hapo panafikika kwa haraka na usafiri sio shidaaaa,"amesema Msama.

Kwa mujibu wa Msama, viwanja vya posta ni katikati zaidi na panaweza kufikiwa na watu wa pande zote za jiji la Dar es salaam na ni eneo ambalo linafikika kirahisi .

Amesema tayari mikoa Saba imethibitisha kuandaa tamasha hilo ikiwemo Dodoma, Mwanza, Simiyu Iringa, Mbeya, na Morogoro.

"Tutaongeza mikoa mingine kadiri ya mahitaji yatakavyokuwa ili kuhakikisha watu wote wanaopenda kupata burudani ya muziki wa injili kupitia Tamasha la Pasaka wanafikiwa,"amesema.

Tamasha la Pasaka linatarajiwa kushirikisha wanamuziki wa nchini Tanzania na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Msama, maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na kwamba, mpaka sasa tayari wamekamilisha mazungumzo na muimbaji kutoka nje.

KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi