loader
Picha

Diwani akataa watendaji

DIWANI wa Kata ya Bukoko Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Jidashema Lukelesha aliyetuhumiwa kumlinda mkazi wa kijiji cha Mangungu anayedaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi, amewakataa watendaji wa Serikali katika kata yake.

Diwani huyo anatuhumiwa kumlinda kijana Jibungu Chenge anayedaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi ya Mangungu.

Aliwakataa watendaji wake wawili akiwemo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipumbulya Charles Lucas na Mtendaji wa Kata ya Bukoko, Fredrick Masesa kwenye kikao cha ndani kilichoitishwa na Katibu Tarafa wa Igunga ambaye pia ni Ofisa Tawala wa Wilaya ya Igunga Shadrack Kalekayo kwa ajili ya kuzungumzia mambo mawili ya utoro wa wanafunzi na diwani kutoelewana na watumishi.

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichowajumuisha wenyeviti wa vitongoji, viongozi wa madhehebu ya dini, wakuu wa shule zote za kata, wazee maarufu na viongozi wa vyama vyote vya siasa, diwani huyo alisema hataki kufanya kazi na watendaji hao wawili na kumtaka Mkurugenzi awaondoe kwenye kata yake.

Alisema watendaji hao wamekuwa wakifanya mambo ya siasa na kuacha kazi za kuwatumikia wananchi na kudai pia kuwa wamekuwa wakiwakamata wazazi wasiowapeleka watoto wao shule na kuwatoza faini bila kujulikana mahali wanakopeleka fedha hizo.

“Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya katika kikao hiki ndugu yangu Ofisa Tarafa, Shadrack Kalekayo nawaombeni muwaondoe hawa watendaji kwenye kata yangu mkishindwa mimi nitajua jinsi ya kuwaondoa kwani diwani si jina la ukoo,” alisema Jidashema.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa kata hiyo Isanzule Jilala, Nshoma Mwandu na Masele Jilunga walisema diwani wao amekuwa akikosana na watumishi wa serikali wanapotekeleza majukumu yao waliyoagizwa na serikali na kuviomba vyombo vya sheria vimchunguze kwa makini.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Jisesa iliyoko Kata ya Bukoko Mafunda Ntemanya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Igunga alisema diwani huyo amekuwa kikwazo cha kukwamisha shughuli za maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo zinazotolewa na serikali.

Mafunda alibainisha kuwa diwani Lukelesha tayari ameshagombana na Kamati ya Shule ya Jisesa baada ya kuilazimisha kamati hiyo ipitishe jina la mkandarasi wa kujenga vyumba vya madarasa ya shule asiyezingatia ubora.

IDARA ya Habari (MAELEZO) imewataka wadau wa habari kufanya utafiti ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi