loader
Picha

Tanzania yauza mahindi ya bil. 21/- WFP

KATIKA kutekeleza mkataba na Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza kusafirisha mahindi tani 36,000 zilizonunuliwa na shirika hilo.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Vumilia Zikankumba amewaeleza waandishi wa habari kuwa, mpaka sasa NRAF tayari imeshasafirisha mahindi takribani tani 15,000 kwenda Uganda.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkataba wa mauziano ya mahindi ulioingiwa kati ya NRFA na WFP, Januari 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Rais John Magufuli ambapo awamu ya kwanza WFA imenunua tani 36,000 kwa Sh bilioni 21.

Mahindi hayo ni sehemu ya tani 160,000 za chakula zenye thamani ya Sh bilioni 132.2 zilizonunuliwa na WFP nchini Tanzania mwaka 2018, ikiwa ni ongezeko la kutoka Sh bilioni 63.6 zilizotumika kununua chakula katika mwaka 2017.

“Tumeshasafirisha nusu ya mkataba wetu unaotutaka kusafirisha mahindi tani 36,000 ambapo hadi hivi sasa kama mnavyoona hapa shughuli zinaendelea na tayari tumesafirisha nusu ya mkataba tayari tani 15,000 zishakwenda nje ya nchi,” alisema Zikankumba.

Aidha aliwataka wakulima kutumia fursa hiyo ya NFRA, kuuza mahindi kwa WFP kulima kwa wingi na kuzingatia ubora. Naye Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Dodoma, Felix Ndunguru alisema kazi ya kusafirisha mahindi tani hizo 36,000 inaendelea vizuri na kuwa watakamilisha katika muda uliopangwa.

“Hapa Dodoma ni kama sehemu ya kuondokea tunayatoa kutoka katika kanda zetu saba za NFRA nchini, ambazo ni Dar es salaam, Songea, Makambako, Shinyanga, Arusha na Dodoma,” amesema.

Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji Chakula wa WFP, Mahamud Mabuyu amesema hatua ya shirika lake kununua mahindi na nafaka Tanzania limetokana hasa na kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo hazitumii tekinolojia ya Uhandisi Jinsi (GMO) katika kilimo.

Alisema kwa mwaka 2018, WFP ilinunua Tanzania tani 136,000 za nafaka na kati ya hizo, tani 23,000 zilikuwa za zao la mtama, jambo ambalo limefungua mlango wa kununua nafaka hiyo hapa nchini.

Mabuyu alisema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mkataba huo, WFP imenunua tani 36,000 za mahindi ambazo zitapelekwa maeneo ya Sudani Kusini na Uganda na kwenye makambi ya wakambizi yaliyopo hapa nchini.

Aidha, Mabuyu amesema katika kusaidia kuinua kilimo cha Tanzania hususani wakulima wadogo, WFP limeweza kuwaunganisha wakulima wadogo 53,000 na NRFA na asilimia 44 ya hao ni wanawake hivyo wamechangia kuwawezesha wanawake wa kitanzania.

Meneja wa Kituo cha Dodoma katika Shirika la Reli Tanzania (TRC) Rose Gauga alisema wanashukuru hatua ya Rais Magufuli kuagiza shirika hilo kushiriki kusafirisha mzigo huo.

Alisema shirika lake lina uwezo mkubwa wa kusafirisha mzigo huo kwani lina mabehewa 140 ya kusafirishia mizigo huku kila behewa likiwa na uwezo wa kubeba tani 40 na kuwa linasafirisha mahindi hayo hadi Uganda ikiyatoa katika Kanda za Dar es Salaam, Shinyanga, Mpanda na Dodoma. Hivi karibuni WFP ilitoa msaada wa Sh bilioni 1.8 kwa TRC kwa ajili ya kukarabati mabehewa 40 ya treni ili kuharakisha

VIONGOZI wa vyama vya siasa vilivyosaidia ukombozi katika nchi zilizopo ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi