loader
Picha

SMZ kujenga ofisi Dodoma

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekabidhi hati ya kiwanja kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ally Idd chenye ukubwa wa ekari 30 kwa ajili ya kujenga ofisi  za serikali hiyo jijini Dodoma.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi jijini hapa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Masuala ya Muungano.

Akizungumza wakati akikabidhi hati hiyo Samia alisema hati hiyo inatolewa, ikiwa ni ukaribisho wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhamia Dodoma.

“Sisi tumeshahamia Dodoma, wizara zote, mawaziri, Makatibu wakuu wapo Dodoma na ujenzi wa wizara unaendelea katika Mji wa Serikali Ihumwa na nadhani mwishoni mwa mwezi huu wizara zitahamia huko,” alisema Samia.

Aliongeza: “Mmekabidhiwa ardhi hii, ni imani yangu tutaanza kuona pilikapilika za kuanza kujenga ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar maana ndiye Mratibu wa masuala ya Muungano na hata ofisi iliyopo Dar es Salaam inayoratibu masuala ya Muungano itahamia Dodoma.”

Awali akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema ukubwa wa kiwanja hicho ni sawa na viwanja 10 vilivyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za wizara za Jamhuri.

“Utoaji wa kiwanja hiki ni utekelezaji wa maelekezo aliyotatoa Rais John Magufuli la kutayarisha eneo, kulipanga na kulipima kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na tulishatoa pia kwa mabalozi wa nchi mbalimbali,” alisema Lukuvi.

Kamati ya Pamoja ya Kushughulikiwa Masuala ya Muungano inakutanisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa lengo la kujadili kujadili masuala mbalimbali ya Muungano.

Akizungumzia kikao hicho, Samia alisema: “Kwa mawaziri wapya najua mtapata uzoefu, kikao hiki kimekuwa kikifanyika na kujadiliana masuala ya Muungano kirafiki kama ndugu moja, yale yaliyokubaliwa yanaenda kwa ajili ya utekelezaji na yale ambayo hayajafikia makubaliano tunarudi tena kwa wataalamu wetu kuangalia upya.”

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alisema kikao hicho ni cha kawaida kilichotanguliwa na vikao vya Sekretarieti, Makatibu wakuu na Mawaziri.

Serikali ilitangaza kuhamia Dodoma mwaka 2016 na takwimu za hadi Desemba 8 mwaka jana zilionesha kuwa watumishi 6,531 kati ya watumishi takribani 7,000 wa wizara zote tayari walikuwa wamehamia Dodoma ikiwa ni sawa na asilimia 87.5.

Awamu ya kwanza ya watumishi 1,789 walihamia Dodoma mwaka 2016 wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na kufuatiwa na awamu ya pili ya kati ya Novemba, 2017 watumishi 2,130 walihamia wakiongoza na Makamu wa Rais, na tayari awamu ya tatu imehamia kati ya Machi na Juni, ikijumuisha watumishi 2,612.

Aidha, Serikali ilimetoa Sh bilioni 1 kwa kila wizara kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za wizara ujenzi katika eneo la Ihumwa ambao kwa

VIONGOZI wa vyama vya siasa vilivyosaidia ukombozi katika nchi zilizopo ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi