loader
Picha

Wafanyabiashara watishia kuvamia barabara

WAFANYABIASHARA wa mboga, samaki na matunda wa masoko ya Tambukareli na Bonanza jijini Dodoma wamelalamikia kukosekana kwa usimamizi wa kauli zinazotolewa katika uendeshaji wa masoko hayo, kiasi cha kukwamisha ufanisi katika biashara zao na hivyo kutishia ustawi wao na wa familia zao.

Kupitia umoja wao wamesema kama hakutakuwa na mabadiliko watalazimika kuvamia barabara kadhaa kufanya biashara. Walizitaja barabara hizo kuwa ni za Uhindini, Nunge hadi Jamatini.

Wafanyabiashara hao walisema jana kwamba jiji limekosa mpangilio wa usimamizi, limekuwa dhaifu katika kusimamia sheria na kanuni za masoko kwa wafanyabiashara ili kuwepo na nafasi ya kufanya biashara.

Imeelezwa pamoja na kukosekana kwa mpangilio kuna mkanganyiko katika maelekezo na matamko ya mara kwa mara yasiyokuwa na majibu kwa wafanyabiashara wa masoko hayo mawili.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara katika masoko hayo mawili, Goha Magwai akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika katika soko la Bonanza lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, alisema wafanyabiashara wa masoko hayo chini ya uongozi wake wanakusudia kuingia na kuzifunga barabara kadhaa kwa ajili ya kufanya biashara ili kunusuru maisha ya familia.

Alisema halmashauri hiyo ya Jiji imekuwa ikitoa maagizo yake tangu mwaka 2009 mpaka 2019 siku ambayo ilitolewa amri kuwa magari yote ya bidhaa za matunda na mbogamboga yaende kushusha bidhaa ili kuuzwa kwa jumla katika masoko hayo.

“Hivyo basi kwa kuwa utekelezaji huo umekuwa wa kudanganyana na sisi acha tukapange biashara hizo kwenye maeneo hayo, ili tuweze kwenda sambamba na wafanyabiashara wengine ambao wameachwa kufanya biashara zao hapa pamoja na kupatiwa maelekezo na uongozi wa jiji,” amesema.

Katibu wa Umoja huo, Saidi Idd alisema kuwa kwa kipindi kirefu uongozi wa Jiji umeshindwa kutekeleza maagizo na kanuni kutokana na kuendelea kuruhusu wafanyabiashara wengine kufanya shughuli zao katika maeneo ambayo yamezuiwa.

Idd alisema kutokana na hali hiyo wafanyabiashara wa masoko hayo ya Tambukareli na Bonanza wamezidi kudumaa kiuchumi na kushindwa kufikia malengo.

“Uongozi wa Jiji umekuwa ukitoa ahadi hewa kwa wafanyabiashara wa masoko yetu haya kwa kutuambia matunda yatashushiwa kwenye soko la Bonanza na mboga soko la Tambukareli, lakini hadi leo hii magari hayo yanashushia pale kwenye soko la Sabasaba,” amesema.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema kuwa ameshatoa agizo hilo tayari la kuwataka wafanyabiashara wa jumla kushusha mizigo yote ya matunda na mboga soko la Bonanza kwa kuwa nafasi ya kutosha ipo.

Amesema masoko hayo ya Bonanza na Tambukareli miundombinu yake ipo katika hali nzuri na kuna maeneo ya kutosha kwa ajili ya mizigo ya jumla kufuatia kurejeshwa kwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa yamevamiwa na watu binafsi.

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi