loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni hizi za mafuta zipongezwe

TAARIFA kwamba kuna kampuni 8 za mafuta nchini zilizoonesha nia ya kuwekeza Tanga kutumia fursa za bomba la mafuta linalotoka Uganda hadi bandari hiyo, ni habari za kufurahisha.

Tunasema ni za kufurahisha kwa kuwa hii itasaidia kupata mafanikio yaliyokusudiwa katika uwekezaji kwenye bomba hilo, ikiwamo ya kuwapatia wananchi wa Tanzania nafasi zaidi za kujiinua kiuchumi.

Habari hizi zinafurahisha zaidi kwa kuwa kampuni zinazotaka kuwekeza ni za hapa nyumbani, kukiwa na maana kubwa zaidi kuwa faida za biashara wanayoweka pale itabaki nchini.

Kampuni zilizotajwa ni pamoja na Tiper waliochukua hekta 100, Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) hekta 300, Kampuni ya GBP hekta 199, Mihan Gas hekta 100, Simba Oil ekari 50, Ngorongoro Petroleum hekta 100, wakitupa hali Watanzania kujivuna kwamba tunajua namna ya kutumia fursa ambazo zipo.

Kiukweli wakati huu ambapo serikali za Tanzania na Uganda zikiwa katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda kuja Tanzania uwekezaji huu uliokusudiwa eneo la Chongeleani jijini Tanga ni furaha tupu katika hesabu za kiuchumi.

Ikumbukwe kwamba huu ni mradi mkubwa kwa mataifa ya Afrika Mashariki na kutokana na uwekezaji huo kama eneo lililotengwa kwa uwekezaji lisipotumiwa zaidi na kampuni za hapa nchini, hali ya baadae ya kihesabu inaweza kuwa mbaya.

Ndio kusema eneo hilo la Chongoleani ambalo Halmashauri ya Jiji la Tanga imetenga ekari zaidi ya 2,000 kwa ajili ya shughuli za uwekezaji, linapokuwa na idadi hii ya wawekezaji wakubwa wa hapa nchini ni hamasa mpya za kiuchumi, ikiwamo ajira za majirani na eneo hilo.

Ajira hizi si lazima ziwe za kuajiriwa na kampuni hizo, lakini hata huduma zinazohitajika na wafanyakazi wa kampuni hizo, ni kichocheo kizuri kwa uchumi wa Tanga na pia taifa kwa ujumla.

Kama alivyosema Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Ramadhani Mposi katika mkutano wake na wadau wa bandari ya Tanga na wafanyabiashara wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha na Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), uwekezaji huo ni mkubwa na watanzania lazima kuuchangamkia.

Tunachoomba ni kwamba wawekezaji hao wafanye haraka kulipia fidia kwa wananchi kama walivyofanya Mamlaka ya Bandari yenyewe ambayo imechukua eneo la hekta 500 na tayari wameshalipa fidia.

OFISA Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore, anatarajia kuachiwa wadhifa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi