loader
Picha

TSN kudhamini tuzo ya Meya Bora

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajia kurejesha Tuzo ya Meya Bora, itakayodhaminiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Aidha, ALAT imeweka mkakati wa kujenga jengo la kitega uchumi baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi ndogo eneo la Tambukareli baada ya mwisho wa mwezi huu.

Mratibu wa Tuzo ya Meya, Wilman Ndile amesema jijini Dodoma kuwa, uzinduzi wa tuzo hiyo unatarajia kufanyika Juni, mwaka huu katika Jiji la Mwanza.

Amesema tuzo hiyo ambayo itadhaminiwa na TSN imelenga kuhamasisha manispaa kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali.

TSN ni mchapishaji wa agazeti ya Daily News, Sunday News, Habari- Leo, HabariLeo Jumapili na gazeti la michezo la SpotiLeo.

Ndile amesema mchakato wa uteuzi katika mashindano utahusisha umma wa Watanzania ambao watatuma ujumbe mfupi wa simu za mikononi kuteua halmashauri bora, majaji watatembelea manispaa husika kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuchagua manispaa bora.

Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulam Mkadam ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga, alisema jengo hilo la kitega uchumi wanatarajia kulijenga karibu na ofisi za ALAT Makao Makuu.

Mkadam ambaye alitembelea eneo la mradi ambapo zinajengwa ofisi ndogo, aliwahimiza wanachama wa ALAT ambao ni pamoja na Halmashauri za Jiji, Wilaya na Miji kukamilisha michango yao ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya jumuiya hiyo.

“Michango ndiyo itakayosaidia kukamilisha miradi yenye thamani ya Sh bilioni nane wa ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litatumika kama kitega uchumi na Makao Makuu ya ALAT,” amesema.

Aidha, Mkadam alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais John Magufuli kwa ahadi yake ya kuunga mkono mradi wa ujenzi

VIONGOZI wa vyama vya siasa vilivyosaidia ukombozi katika nchi zilizopo ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi