loader
Picha

Wanaofungua milango ya wananchi usiku wadakwa

JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu, ikiwemo wizi wa kutumia funguo za bandia kwa kufungua milango ya wananchi wanapokuwa wamelala nyakati za usiku.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga, Ally Mkalipa alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Igunga katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sokoine, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kuimarisha ulinzi shirikishi.

Mkalipa alisema katika msako unaoendelea Wilaya ya Igunga wa kuwasaka baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu wamefanikiwa kukamata kundi la vijana ambalo hakutaja idadi wala majina yao, wakiwa na funguo zaidi ya 1,000 wanazofanyia uhalifu.

Alisema katika funguo hizo zipo ambazo zinatumika kufungua milango ya aina ya vitasa ambazo zimetengenezwa kwa kutumia nondo na kuongeza kuwa baada ya kuwakamata walipowahoji walikiri kufanya uhalifu maeneo mengi. Sambamba na hayo, Mkalipa alitoa tahadhari kwa wananchi wanaopanda pikipiki kwa kukodi kuwa makini kwa kuwa wapo baadhi ya waendesha bodaboda si waaminifu ambao wamekuwa wakitumia namba za pikipiki tofauti wanapokodiwa kuwasafirisha abiria.

Aliwataka wananchi na wafanyabiashara kuimarisha milango yao na kuajiri walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo, ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara mizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Igunga kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ili kukomesha vitendo vya uhalifu kwa kuimarisha ulinzi.

Kuanzia kesho Alhamisi, kimbunga kilichopewa jina la Kenneth kitakuwa umbali ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi

TMA yataja maeneo yatakayoathiriwa na kimbunga Kenneth

masaa 5 yaliyopita Na JANETH MESOMAPYA

Kuanzia kesho Alhamisi, kimbunga kilichopewa jina la Kenneth kitakuwa umbali ...

Mwandishi kutoa ushahidi kesi ya Halima Mdee

masaa 7 yaliyopita Mwandishi kutoa ushahidi kesi ya Mdee Na Francisca Emmanuel MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemtaka Mwandishi wa Kampuni ya Clouds Media, Abdi Chembeya kufika mahakamani hapo Mei 14, mwaka huu kutoa ushahidi katika kesi ya uchochezi inayo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemtaka mwandishi ...

Mkuu IFM kuongoza bodi Wakala wa Meli

masaa 8 yaliyopita Mwandishi Maalum

RAIS John Magufuli amemteua Profesa Tadeo Andrew Satta kuwa Mwenyekiti ...