loader
Picha

Mwenyekiti, mgambo mbaroni kwa mauaji

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Bangata, wilayani Arumeru, Michael Silamoi kwa tuhuma za kumshambulia hadi kumsababishia kifo mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho.

Mbali na Mwenyekiti huyo, wengine wanaoshikiliwa ni askari mgambo wawili wa kijiji hicho waliofahamika kwa majina ya Balozi Andrea na Wariael Obedi pamoja na mkazi mwingine aliyefahamika kama Onesmo Siyoi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), Hassani Omary akizungumza na gazeti hili jana alithibitisha Mwenyekiti huyo na wenzake watatu kuendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa tangu kukamatwa kwao Januari 8, mwaka huu.

“Ni kweli Mwenyekiti wa kijiji cha Bangata na wenzake watatu tunaendelea kuwashikilia kwa tuhuma za kumpiga hadi kusababisha kifo cha Stalei Samwel (29) kilichotokea Januari 3, na jalada la kesi hiyo tumeshalipeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema.

Mkuu huyo wa Upelelezi wa Mkoa wa Arusha aliongeza kuwa watuhumiwa hao hawawezi kuachiwa kwa dhamana kutokana na kuwa wanatuhumiwa kwa mauaji na kinachosubiriwa ni taratibu zikamilike ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.

Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo, baba mzazi wa marehemu huyo, Samwel Lukumay (77), alisema kuwa kijana wake alikamatwa na mwenyekiti huyo akiwa na watuhumiwa hao wanaoshikiliwa na Polisi pamoja na mwenyekiti wa usalama wa kijiji hicho, Nuruel John ambaye alitoroka baadaye.

Alisema kuwa kijana wake alifungiwa katika ofisi ya kijiji na kuanza kushambuliwa na watuhumiwa hao na kwamba chanzo cha tukio hilo ni mwanawe kudaiwa kumjeruhi mmoja wa wanakijiji.

Alisema viongozi hao walimjeruhi mwanawe sehemu mbalimbali za mwili wake na kufikia kumnyoa nywele zake kwa kutumia panga, hali iliyosababisha hadi ngozi ya kichwa kutoka.

Mzee huyo aliongeza kuwa baada ya viongozi hao kuona hali ya kijana wake ni mbaya walimpeleka katika Kituo cha Polisi Baraa wakidai kuwa alikuwa ni mwizi na kwamba alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali jambo ambalo polisi walilitilia shaka na kutoa PF3 ili akapatiwe matibabu kutokana na hali yake aliyokuwa ambapo alifariki

IDARA ya Habari (MAELEZO) imewataka wadau wa habari kufanya utafiti ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi