loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gereza ambalo wafungwa wanalazimika kutafuta kazi

GEREZA la wazi la Sanganer lililoko katika mji wa Jaipur nchini India, wafungwa wanapewa mahala pa kulala lakini hawapewi fedha wala chakula. Hii inamaanisha kwamba wanapaswa kwenda kufanya kazi nje ya milango ya gereza ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao wakiwa gerezani... Endelea na makala haya yaliyoandikwa na Masuma Ahuja wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC).

Ramchand anaendesha basi la shule. Mkewe, Sugna, anafanya kazi katika kiwanda cha nguo. Hivi karibuni niliwatembelea wawili hao na kunywa chao nao wakiwa katika nyumba yao ya chumba kimoja yenye kuta za njano na paa la bati.

Pale chumbani kwao kuna friji na TV, sanduku la kutunzia chakula likiwa limening’inia kwenye kona moja karibu na picha za Miungu wao na pia kuna magazeti kadhaa. Kupotia mlangoni mwa chumba chao, unaweza kuona magari yanayopita katika upande mmoja wa barabara, na unaweza kuona jengo moja la kisasa la ghorofa kwa mbali. Chumba chao kinaonekana cha kimaskini na huwezi kukizungumzia sana na hata wao hawana mengi ambayo wanaweza kukusimulia kuhusu uhusiano wao lakini ukweli ni kwamba wawili hao, Ramchand na Sugna ni wafungwa.

Wote wawili walipatikana na hatia ya mauaji na hapo walipo wako jela. Chumba chao ni moja ya vyumba vya wafungwa katika gereza la Wazi wa Sanganer, Jaipur ambao ni mji mkuu wa jimbo la magharibi la India la Rajasthan. Gerezani hili halina nondo wala kuta ndefu. Hakuna walinzi wa usalama katika lango, na wafungwa wanaruhusiwa - hasa wanahamasishwa - kwenda nje ya gereza hilo kutafuta na kufanya kazi kila siku.

Gerezani hili lina wafungwa wapato 450 na ni moja ya kati ya magereza 30 yaliyomo katika jimbo hilo la Rajasthan. Mimi (mwandishi wa makala haya) nilienda Sanganer nikiwa na Smita Chakraburtty, mwanamke aliyeanzisha kampeni ya kuanzishwa kwa jela wazi nchini India. Ameendelea kuishawishi Mahakama ya juu kabisa ya India, ambayo imekuwa ikikubaliana na hoja zake na sasa mahakama hiyo imekuwa ikiibana serikali kuanzisha magereza mengi zaidi kama haya.

Chakraburtty sasa anaitwa kamishna wa heshima wa magereza katika jimbo la Rajasthan, na hivi karibuni alichaguliwa kuwemo kwenye watu wanaogombea Tuzo ya Agami ya India ambayo hutolewa kwa mtu anayejitoa katika masuala muhimu kwa maisha ya wananchi. Yeye amependekezwa kupewa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake katika kubadili mfumo wa adhabu nchini India. “Mfumo wa utoaji haki kwa makosa ya jinai wa India huzungumzia tukio lakini haujui nini cha kufanya dhidi ya mtu binafsi,” Chakraburtty anasema.

Msimamo wake umesababisha majimbo mengine manne nchini India kuanzisha magereza mapya ya wazi hususani mwaka jana. Ninapotembelea Sanganer na Chakraburtty anawapa wafungwa habari za hivi karibuni juu ya kazi zake, na kisha wananigeukia mimi wakipenda kuzungumza na mwandishi wa habari. Yote haya yanafanyikia gerezani huku kukiwa hakuna walinzi na mtu yeyote anaweza kuingia gerezani bila kizuizi ingawa wageni kama mimi ni wachache.

Baadaye ninakaa sakafuni katika shule ya watoto wa chekechea mbele ya gereza na kuzungumza na kundi la wanaume na wanawake ambao ni wafungwa. Ninapowauliza kwa nini wamefungwa gerezani, wengi wanasema ni kutokana na “302,” wakimaanisha kifungu cha 302 katika Kanuni ya Adhabu ya India ambacho kinaamuru adhabu ya kifungo kwa anayepatikana na hatia dhidi ya mauaji.

Wao wanaliiita gereza hilo la wazi kuwa ni “Shamba,” na wanaeleza jinsi ilivyo rahisi kuishi na humo na jinsi wanavyofurahi. Ili mtu apelekwe kuishi katika gereza la Sanganer, anapaswa awe ameshahudumia angalau theluthi mbili ya kifugo chake katika magereza yaliyozungushiwa kuta ndefu na nondo na wafungwa hawa unapowauliza kulinganisha magereza walikotoka na hilo la Sanganer wanajibu kwamba hapo wanajiona kama wako uhuru. Inaelezwa kwamba serikali ya jimbo la Rajasthan ililazimika kuwafukuza wafungwa ambao walimaliza vifungo vyao lakini wakawa hawataki kuondoka katika gereza hilo la wazi.

Hii ni kutokana na kwamba walikuwa wameanzisha maisha hapo ya kudumu kwa maana ya ajira imara, shule za watoto wao na hivyo hawakutaka hata vifungo vyao kumalizika. Hata hivyo, wafungwa wengi wananiambia wanapambana katika kubadlisha mtazamo wa watu ya nje ya gerezani. Wanawake wafungwa wanasema ni rahisi kuolewa na mwanaume mfungwa, kwa sababu wanaume nje ya gerezani hawaelewi uzoefu wao.

Hata wanasema wakati mwingine kupata kazi ni ngumu kwani kuna wanaosita kuwaajiri baada ya kuona vitambulisho vikionesha kwamba wao ni wafungwa walio katika gereza la wazi. Hata hivyo bado wafungwa wengi wanaishi maisha ya kawaida hapa Sanganer: wananunua pikipiki, simu janja na televisheni. Hawavai sare za jela kama wafungwa wengine na waishi katika nyumba ndogo ndogo.

Kila mfungwa anapewa chumba na serikali lakini hawapewi chakula, maji au kipato chochote. Kwa hiyo kila siku, wengi wao huondoka kwenye eneo la gereza ili kutafuta maisha: wanaume wengi waliopatikana na hatia za mauaji wanajihusisha na kazi za ulinzi, vibarua kwenye kiwanda na kazi zingine za kutwa. Nilikutana na mfungwa mmoja ambaye ni mwalimu wa mazoezi ya viungo na mwingine ni mwalimu katika shule ya karibu na gereza. Amri pekee kwa wafungwa hawa ni lazima kila jioni wawepo gerezani na kuitwa majina (roll call). Kwa kweli ni vigumu kujua Sanganer ni gereza hadi unapofika wakati huu ambao wanafoleni ili kuhesabiwa kwa kuitwa majina kwenye mlango wa gerezani. Mtumishi wa gereza aliye na kipaza sauti huanza kuchukua mahudhurio, akitoa namba kutoka 1 hadi 450.

Wakati mwingine, husimama anapoita jina fulani na kumfokea mfungwa kwa kuacha takataka nje ya nyumba yake. Mwishoni mwa mwaka 2015, takwimu zilizotolewa zilionesha kwamba kati ya wafungwa 419,623 walioko nchini India, 3,789 (sawa na asilimia 0.9%) walikuwa katika jela za wazi Majimbo mawili ya Rajasthan na Maharashtra yana jumla ya magereza 42 ya wazi - zaidi ya nusu ya magereza yote ya aina hiyo nchini India. Makala haya yametafsiriwa kwa Kiswahili na Hamisi Kibari yaliyotoka kwa mara ya kwanza katika Jarida la

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka ...

foto
Mwandishi: BBC

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi