loader
Picha

Simba yapewa mbinu kuimaliza Al Ahly

KOCHA na nyota wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema Simba inatakiwa kushambulia ili kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly kesho.

Simba itarudiana na mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa ni kipindi cha wiki moja tangu wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika ngazi ya klabu kukubali kipigo cha mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa Alexandria, Misri.

Hicho kilikuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ambao kabla ya mechi hiyo walitoka kufungwa idadi kama hiyo ya mabao na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) mchezo uliochezwa jijini Kinshasa.

Matokeo hayo ya wekundu hao wa Msimbazi yalimuibua mkongwe Abdallah Kibadeni ambae mbali na kuwahi kuichezea kwa mafanikio makubwa klabu hiyo, lakini pia amewahi kuifundisha kwa mafanikio makubwa na kuwashauri wachezaji soka la kushambulia kama watahitaji kupata ushindi.

“Hauwezi kusema waingie uwanjani kwa lengo la kujihami kwa sababu lengu letu sisi ni ushindi; tumefungwa mechi mbili, tena kwa idadi kubwa ya mabao. Hakuna namna zaidi ya kucheza soka la kushambulia na kutumia kila nafasi itakayopatikana.

“Washambulie kwa nidhamu kubwa huku pia wakikumbuka majukumu ya kuzuia na kutowaruhusa Al Ahly kupata bao,”alisema Kibadeni ambae aliiongoza Simba kufika fainali ya kombe la Shirikisho la Soka la Afrika(CAF) mwaka 1993.

Kibadeni aliyekuwa kocha wakati Simba inaifunga Al Ahly mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mwaka 1985, alisema kwa kuwa wanacheza kwenye uwanja wao wa nyumbani Simba hawana budi kujituma kupata hata ushindi mwembamba utakaotoa matumaini kufuzu kwenye hatua ya robo fainali.

Nguli huyo aliwashauri Simba kwa msimu ujao kuunda timu yenye wachezaji wenye ubora hasa kutoka Tanzania na nyota wageni waje kuongeza ushindani.

“Shida katika soka letu siku hizi kila mtu mjuaji lakini Simba ina watu wengi wanaoweza kuwajumuisha kwenye benchi lao la ufundi na kutoa ushauri mzuri utakaoisaidia timu hiyo,” amesema.

Kibadeni amewataja nyota wa zamani wa timu hiyo kama vile Khalid Abeid, Mtemi Ramadhani na Emmanuel Albert Mbele kama ni watu wenye uwezo wa kuisaidia kimawazo timu hiyo.

Simba inashika nafasi ya tatu kwenye kundi D ikiwa na pointi tatu na mabao matatu ya kufunga baada ya kucheza michezo mitatu kwenye kundi lake.

KOCHA wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi