loader
Picha

Beki kisiki Al Ahly kuwakosa Simba

WASHAMBULIAJI wa Simba huenda wakakutana na nafuu baada ya wapinzani wao Al-Ahly kuthibitisha kumkosa beki wao tegemeo, Saad Samir ambaye alimdhibiti vilivyo Meddie Kagere katika mchezo uliofanyika nchini Misri wiki moja iliyopita.

Msafara wa mabingwa hao wa zamani wa Afrika uliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana bila ya beki huyo aliyewadhibiti vilivyo washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere kwenye mchezo ambao Simba walifungwa mabao 5-0.

Saad Amir ni beki mwenye uzoefu wa mashindano mbalimbali aliwahi kucheza mechi za kufuzu Kombe la Dunia kwa miaka kadhaa na Kombe la Mataifa ya Afrika na amekuwa akitegemewa katika idara ya ulinzi ya timu hiyo kutokana na uwezo wake wa kukaba na kupandisha mashambulizi.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika wanaongoza katika kundi D wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na As Vital wenye pointi 4, Simba ina pointi tatu na Js Saoura ikiwa na pointi mbili baada ya kutoa sare michezo miwili na kupoteza dhidi ya Simba.

KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi