loader
Picha

Kocha Mtibwa atamba kuinyuka Mwadui

KOCHA wa Mtibwa Sugar ya Morogoro Zuberi Katwila ametamba kuishushia kipigo Mwadui ya Shinyanga kwenye mchezo utakaopigwa leo katika dimba la CCM Kambarage.

Mtibwa Sugar imekuwa ikipata matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi zake za hivi karibuni ambapo kwenye mchezo uliopita walitoka sare ya bao 1-1 na African Lyon.

Mpaka sasa Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 21 na kujinyakulia pointi 29, wakishinda michezo minane, kutoka sare michezo mitano na kufungwa mara nane.

Katwila aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa hawana muda tena wa kupoteza mechi zao na wamefanya maandalizi ya kutosha yatakayowafanya waibuke na ushindi dhidi ya Mwadui.

“Nikwambie tu mipango ya kikosi changu iko sawa na wachezaji wangu wana ari kubwa ya kupata matokeo kwenye mchezo wetu kesho (leo),“ amesema Katwila.

Amesema ushindi kwao ni muhimu ili kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kwani upinzani ni mkali kwa kila mechi wanayocheza.

Baada ya mchezo dhidi ya Mwadui, Mtibwa wataelekea mkoani Mara tayari kuwakabili Biashara United kwenye muendelezo wa mechi zao za Ligi Kuu.

KIPA wa Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi