loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona, Liverpool zabanwa

MATOKEO ya suluhu, yaani bila ya kufungana ndio yalitawala juzi katika mechi za hatua ya 16 bora za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Liverpool wakiwa nyumbani dhidi ya timu ya Ujerumani ya Bayern Munich walijikuta wakilazimishwa sare ya bila kufungana kwenye uwanja wao wa Anfield katika mchezo wa kwanza, huku vigogo Barcelona nao walibanwa na kujikuta wakitoka suluhu dhidi ya Lyon katika mchezo mwingine wa michuano hiyo.

Barcelona sasa itabidi kusubiri kufanya mambo katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kwenye uwanja wao wa Nou Camp Jumatano Machi 13.

Katika mchezo wa Liverpool, wenyeji walikuwa tishio lakini walishindwa kutumia nafasi nzuri za kufunga baada ya kufika mbele ya lango mara kadhaa na kukumbana na safu ya ulinzi ya Bayern Munich iliyokuwa imara.

Sadio Mane alikosa nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha kwanza baada ya kupiga shuti juu ya lango akiwa ndani ya eneo la penalty huku akiwa hajakabwa. Joel Matip naye pia alishindwa kufunga baada ya krosi safi ya Roberto Firmino akiwa ndani ya meta sita katika lango la wapinzani, lakini alipiga nje.

Baada ya hapo, Matip nusura aipatie Bayern Munich bao la mapema la ugenini wakati aliposhindwa kuujaza wavuni mpira uliopanguliwa na kipa wa Liverpool Alisson na kurudi uwanjani.

Mabingwa hao wa Ujerumani walicheza vizuri katika safu ya ulinzi katika kipindi cha pili, huku Mane akikaribia kufunga kwa kichwa katika dakika ya 85, lakini mpira huo uliokolewa.

Mchezo wa marudiano wa timu hizo utafanyika kwenye Uwanja wa Allianz Arena utakaofanyika Machi 13. Kirekodi Bayern Munich imepoteza michezo miwili tu kati ya 26 iliyocheza nyumbani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, lakini Liverpool watakuwa na faida mara mbili endapo watafunga katika mchezo huo wa ugenini.

Ikiwa Liverpool itatupwa nje, watajilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi kwenye uwanja wa Anfield.

Kwa upande wa Barcelona wenyewe itabidi wajilaumu baada ya kushindwa kutumia nafasi kibao walizopata na kujikuta wakilazimishwa suluhu katika hatua hiyo ya 16 bora dhidi ya Lyon.

Mara kibao, nyota wa Barca Lionel Messi, Luis Suarez na Phillipe Coutinho walishindwa kufunga baada ya kupata kikwazo kutoka kwa kipa wa Lyon, Anthony Lopes. Lyon nayo ilipata nafasi pia, lakini Marc-Andre ter Stegen na Martin Terrie mashuti yao ya mbali yaliishia kugonga mtambaa `panya’.

Timu hizo zitarudiana kwenye Uwanja wa Nou Camp Jumatano ya Machi 13. Barca ambao ni mabingwa wa La Liga na wanaongoza hadi sasa katika msimamo, wako pointi saba kileleni mwa ligi hiyo mbele ya Atletico Madrid iliyopo katika nafasi ya pili, lakini timu hiyo haijawahi kushinda katika mashindano makubwa ya Ulaya tangu mwaka 2015 wakati walipofungwa na Juventus katika fainali.

OFISA Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore, anatarajia kuachiwa wadhifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi