loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

R Kelly ashitakiwa udhalilishaji kingono

MSANII mahiri wa Marekani, R Kelly ameshitakiwa kwa makosa 10 akidaiwa kuhusika kuwadhalilisha kwa ngono takribani wanawake tisa na watoto.

Nyota huyo wa R&B, ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, anakabiliwa na makosa hayo anayotuhumiwa kufanya dhidi ya wanawake na watoto wenye umri mdogo.

Huko nyuma hakuwahi kupatikana na hatia licha ya kuwahi kutuhumiwa na makosa kama hayo, alikana tuhuma zote.

Hati ya kumkamata ilitolewa, na msanii huyo mwenye umri wa miaka 52 alijipeleka mwenyewe polisi, huko Chicago baadae juzi Ijumaa.

Mwanasheria wake anasema mteja wake alishtushwa na tukio hilo. Steve Greenberg aliliambia Shirika la Habari la Associated Press (AP) kuwa mteja wake “alisikitishwa sana na kushtushwa” na mashtaka hayo na anasisitiza kuwa ahusiki na madai hayo.

Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya msanii huyo kurusha hewani vipindi kadhaa vya Surviving R Kelly.

Tuhuma zilibeba madai kibao ya miongo kadhaa dhidi ya R Kelly, kutoka kwa wanawake, akiwemo mke wake wazamani. MADAI GANI ? Waendesha mashtaka walitangaza kuwa msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya jinai ya udhalilishaji wa kijinsia, waathirika wanne wakihusika.

Walisema kuwa matukio hayo yalitokea kati ya mwaka 1998 na 2010. Taarifa zinasema angalau waathirika walikuwa na umri kati ya miaka 13 na 16 wakati matukuio hayo yakiripotiwa.

Mwanasheria wa mahakama ya Cook County Kim Foxx alisema msanii huyo anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka saba jela kwa kila kosa. Hakuna dhamana iliyotolewa kwa Kelly hadi sasa.

Greenberg, mwanasheria wake, aliliambia Shirika la Habari la AP kuwa amepewa nafasi ya kukaa pamoja na waendesha mashtaka kabla ya kuandika barua kuelezea kwanini `mashtaka hayo hayana msingi’ lakini alisema walikataa.

Mwanasheria wa Cook County, Kim Foxx aliwataka wanawake wote waliofanyiwa unyama na msanii huyo kujitokeza mbele baada ya makala hayo kurushwa hewani.

Mwanasheria Michael Avenatti alisema kuwa yeye anawawakilisha watu sita, wakiwemo mawanawake mawili wanaodaiwa kutoa tuhuma dhidi ya Kelly.

Mwanasheria huyo anasema kuwa tepu au mkanda huo wa dakika 40, anaamini ulirekodiwa mwaka 1999, unamuonesha Kelly akijihusisha na ngono na watoto wenye umri mdogo. Mkanda huo aliuwasilisha kwa waendesha mashtaka.

Pia inaonesha kuwa msanii huyo alikuwa akiifanya mapenzi kinyume cha maumbile na picha nyingine inamuonesha akifanya mapenzi na mtoto w miaka 14.

Mtangazaji wa Kituo cha CNN alisema kuwa aliona picha mpya na kuelezea kuwa zilikuwa zikionesha wazi akifanya vitendo hivyo.

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi