loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Liverpool yarejea kileleni England

LIVERPOOL imerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini pamoja na hayo imejikuta ikichanganyikiwa baada ya kushindwa kuifunga Manchester United na kutoka nayo suluhu juzi, licha ya wenyeji kuwa na majeruhi kibao.

Sare hiyo nyumbani dhidi ya wapinzani wake hao wakubwa, ilikichanganya kikosi cha kocha Jurgen Klopp, baada ya kukosa nafasi kibao za kufunga. Kwa matokeo hayo ya suluhu, Liverpool sasa imefikisha pointi 66, moja zaidi ya Manchester City iliyopo katika nafasi ya pili baada ya timu hizo kila moja kucheza mechi 27, huku Tottenham Hotspur ikishika nafasi ya tatu wakati Arsenal ikiwa katika nne bora baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.

Kuumia kwa viungo wake watatu kulikuwa na maana kuwa, Man United walilazimika kutumia wachezaji wake wote wa akiba ndani ya kipindi cha dakika 25 kabla ya mapumziko, huku mmoja akiwa Jesse Lingard. Liverpool nayo haikuwa `salama’ baada ya Roberto Firmino ambaye alidumu hadi baada ya nusu saa, ambapo bila yeye timu hiyo ilibidi kupambana ili kufanya vizuri katika mbio zake hizo za kusaka bao. Hata hivyo, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao katika kipindi cha kwanza na kile cha pili na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Kikosi cha Klopp kilishindwa kabisa kupenya ngome ya Man United na kumfikia kipa David de Gea, huku wakijaribu kupiga mashuti ya mbali yaliyopigwa na Firmino aliyechukua nafasi ya Daniel Sturridge shuti pekee ambalo lililenga lango katika dakika ya 90. Man United walipata nafasi nzuri katika mchezo huo, lakini Alisson alizuia shuti la Lingard baada ya kukimbia na mpira alipata kutoka kwa Romelu Lukaku ni kujaribu kumzunguka kipa wa Liverpool.

Wakati Manchester City wakicheza mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi (Kombe la Carabao) dhidi ya Chelsea juzi Jumapili na kushinda 2-0, matokeo hayo yana maana kuwa Liverpool imepanda pointi moja juu ya City zikiwa zimebaki me- chi 11 kabla ya kumalizika kwa timu hiyo. Man United imeporomoka hadi nafasi ya tano, huku Arsenal ikipanda hadi katika nafasi ya nne baada ya ushindi dhidi ya Southampton.

MAJERUHI KIBAO Man United ambao haikuwa katika mbio za kusaka ubingwa, huo bado ulikuwa mchezo muhimu kwao hasa kwa kocha wake wa muda Ole Gunnar Solskjaer, ambaye anasaka mkataba wa kudumu. Hiyo ilikuwa nafasi yake ya kuonesha kuwa anafiti kuchukua nafasi hiyo katika mkataba wa kudumu, lakini timu yake imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

OFISA Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Peter Moore, anatarajia kuachiwa wadhifa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi