loader
Picha

Kenyatta atamani Rais mwanamke

RAIS Uhuru Kenyatta amesema anatamani kuona sasa Kenya inakuwa na Rais mwanamke kwa kuwa wameiva kiuongozi.

“Wengi wao wameshaiva kiuongozi. Natamani siku moja Kenya ipate Rais mwanamke. Mawaziri wangu wengi wa kike ni mfano wa kutosha wa jinsi wanawake walivyoiva kiuongozi. Wanafanya kazi kubwa sana,” amesema Kenyatta.

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na maskauti wa kike zaidi ya 2,000 waliokusanyika Ikulu jijini Nairobi kuadhimisha Siku ya Kufikiri Duniani, wakiitikia mwito wa mke wa Rais Kenyatta, Margaret, ambaye ndiye mlezi wa maskauti wa kike nchini humo.

Kama dhamira ya Kenyatta itatimia, mshindi wa kiti cha urais atakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo imewahi kuwa na Makamu wanne tu wa Rais, Samia Hassan Suluhu wa Tanzania na Specioza Kazibwe aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Uganda kati ya mwaka 1994 na 2003, akiwa mwanamke wa kwanza Afrika kushika wadhifa huo.

Wengine ni raia wa Burundi, Alice Nzomukunda na Marina Barampama waliopokezana kijiti cha Umakamu wa Rais kati ya mwaka 2005 na 2006.

Burundi pia imewahi kutoka mawaziri wakuu wawili, Silvie Kinigi kwa siku 109 na Agathe Uwilingiyimana kwa siku 263. Rais Kenyatta, akisisitiza, alisema mbali na watoto hao, wanawake kwa ujumla wao wanapaswa kujiamini na kuthibitisha kuwa wana uwezo wa kufanya lolote sawa na wanaume, na pengine kuwazidi.

Aliwataka maskauti hao wa kike kuonesha uwezo wao wote katika uongozi na mambo mengine wanayoyamudu ili kuuthibitishia umma kuwa, wanawake wanaweza kuwa viongozi bora.

Mke wa Rais Kenyatta, Margaret naye aliwataka wasichana hao kusimama imara katika misingi ya heshima, uzalendo na uongozi na kuwa mfano katika jamii.

Kwa sasa, hasa barani Afrika, ni nchi za Mauritius, Liberia na Ethiopia ndizo zilizowahi kuchagua marais wanawake. Ameenah Gurib- Fakim, mwanasayansi wa Mauritius aliingia ikulu Juni 5, 2015.

SERIKALI nchini Canada imeidhinisha kufanyika kwa majaribio ya kwanza ya ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi