loader
Picha

Dodoma yakaribisha wawekezaji viwanda

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inawaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwa ubia kujenga viwanda vikubwa, vya kati na vidogo ili kupanua huduma katika makao makuu ya nchi.

Hivi sasa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zaidi ya 669.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Godwin Kunambi amesema jiji hilo limejiandaa kupokea wawekezaji kwa kuandaa na kutenga maeneo ya uwekezaji na ujenzi huo wa viwanda.

Amesema halmashauri hiyo kwa kujiandaa huko imefungua milango kwa ajili ya wawekezaji mbalimbali kwa ubia au wao binafsi kujenga viwanda wanavyoweza viwe vikubwa, vya kati au viwanda vidogo.

Amesema wawekezaji wanaweza kujikita katika kujenga viwanda vya kuchakata nafaka kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani na viwanda vya vyakula pamoja na huduma nyingine katika jiji hilo.

Amesema kwa sasa viwanda vikubwa vilivyopo (10) ambavyo vinajumuisha viwanda vya magodoro, machinjio ya wanyama mbalimbali, viwanda vya madini ya ujenzi, viwanda vya maji na juisi na mvinyo pamoja na kusindika mazao, viwanda vya nyama na mafuta ya alizeti.

Amesema hivyo wawekezaji wanaweza kuwekeza katika kujenga viwanda hivyo au kujenga viwanda vingine, kwani tayari jiji limeshaandaa mpango mahususi wa maeneo ya kujenga viwanda hivyo.

“Maeneo ambayo jiji limeandaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo ni pamoja na eneo la Hombolo, Ipala, Mpunguzi, Mbabala, Nala na Chihanga,” amesema Kunambi.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi