loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii wamlilia Ruge

SHIRIKISHO la wasanii Tanzania (Shiwata) imepokea kifo cha Mkurugenzi wa Masoko wa Clouds Media, Ruge Mutahaba kwa majonzi na huzuni kubwa.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Shiwata jana Deo Kway amesema mtandao huo utamkumbuka marehemu Mutahaba kama mwanachama wao mwanzilishi aliyekuwa akimiliki kadi namba 69 aliyoipata mwaka 2006.

Kway amesema wakati wa uhai wake Mutahaba aliwashirikisha wasanii wa kikundi chake cha THT kuwatembelea wenzao wa Shiwata waliojenga nyumba zaidi ya 200 Mkuranga kujifunza ujenzi wa gharama nafuu.

Amesema Mutahaba alikuwa akitoa ushauri kwa Shiwata wakati wa matamasha yaliyosimamiwa na mtandao huo na kushauri wasanii wake kujiunga na bima ya afya kupitia PPF.

Mutahaba alifariki dunia Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa maradhi ya figo na ini na mwili wake unatarajiwa kuwasili nchini leo kabla ya kuagwa kesho na kusafirishwa kwao Bukoba kwa maziko.

WILLIAN ameandika katika mitandao yake ya kijamii kuwa anamaliza miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi