loader
Picha

Miradi ya bil. 7/- kutekelezwa Dodoma, Kigoma

MIRADI 47 ya uwekezaji imeibuliwa na kuanza kutekelezwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC) inayotekelezwa katika halmashauri za mikoa wa Dodoma na Kigoma.

Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk Charles Mhina ameyasema hayo wakati wa kuelezea mafanikio ya mradi huo ambao ulisainiwa Januari mwaka 2015.

Amesema miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 7.019 na kunufaisha watu 18,896 kati ya hayo wanawake ni 6,586 na wanaume 12,310.

Dk Mhina amesema miradi hiyo imelenga katika kuboreshaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, miundombinu ya masoko, minada, machinjio, utafiti wa vyanzo vya maji na viwanda vidogo.

"Pia kupitia mradi huu wafugaji na wakulima wapatao 1,500 wamejengwa uwezo kwa kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali, kuaandikia maandiko ya miradi na kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya kujipatia mikopo ili kukuza mitaji yao.

Alisema pia wamekarabati cha kutuo cha mafunzo ya kilimo na ufugaji kibiashara kwa nadharia na vitendo kwa vijana na wanawake cha Kibakwe Resource Center katika halmashauri za Mpwapwa ambapo wanawake na vijana wapatao 250 wamepata mafunzo.

Dk Mhina amesema pia umewezesha kujengwa kwa vituo 13 vya utoaji huduma za biashara na uwekezaji kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.45 ambavyo vimepunguza urasimu wa utoaji wa huduma za biashara na uwekezaji na kuongeza idadi za biashara na mapato ya halmashauri.

"Kwa sasa mradi unaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, upimaji na utoaji wa hati katika miradi mikubwa ya uzalishaji kupitia kilimo cha umwagiliaji na makazi katika halmashauri za Wilaya za Kasulu na Uvinza mkoani Kigoma na zile za Bahi na Kondoa mkoani Dodoma.

Ameongeza: "Kukamilika kwa mradi huu unaogharimu zaidi ya Sh milioni 596.33 na tunatarajia wakulima na wafanyabiashara zaidi ya 9,266 watanufaika."

Kuhusu eneo la kuboresha miundombinu ya ukusanyaji wa mapato, Dk Mhina amesema LIC wamewezesha kununuliwa kwa mashine za kielektroniki za kukusanya mapato (POS) 235 kwa thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.95.

Amesema fedha hizo zimechangia ongezeko la makusanyo kwenye halmashauri za Mkoa wa Kigoma kwa asilimia 88 katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2018 na kwa asilimia 130 kwa Mkoa wa Dodoma.

"Katika eneo hilo mradi umeiwezesha OR-Tamisemi kukamilisha maandalizi ya mwongozo wa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato katika mamlaka za serikali za mitaa," amesema.

Dk Mhina alisema pia wamefanikiwa kuanzishwa na kuendelezwa kwa mabaraza ya biashara ya wilaya zote za Dodoma na Kigoma.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi