loader
Picha

Trafiki agongwa na gari, afa

ASKARI wa Usalama Barabarani, PC Victor wa Kituo cha Polisi Tarime, mkoani Mara juzi alikufa papo hapo baada ya gari, Nissan Hardbody yenye namba za usajili DFPA 1427 mali ya Halmashauri ya Tarime kumgonga.

Ajali hiyo ilitokea juzi jioni eneo la daraja la Bomani wakati dereva wa gari hilo, Cosmas aliposhindwa kulimudu gari hilo lililokuwa kwenye mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wilayani hapa, ACP Yahaya Mdogo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha kifo cha askari huyo. “Ni kweli tumempoteza askari wetu wa kikosi cha usalama barabarani PC Victor kwenye ajali hiyo, mwili wake umehifadhiwa hospitali ya wilaya kwa uchunguzi zaidi,” alisema Mdogo.

Alisema dereva huyo, Cosmas anashikiliwa kwa mahojiano na hatua za kisheria zaidi. Polisi walisema gari hilo lilikuwa likielekea Bomani na dereva wake alikuwa mwendokasi ndipo akapoteza mwelekeo na kumgonga askari huyo aliyekuwa akiendesha pikipiki kutoka Bomani kwenda mjini alikufa papo hapo.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Samson Chacha,Tarime

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi