loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima walioua mtoto wafungwa

MAHAKAMA Kuu Afrika Kusini imewahukumu kwenda jela wakulima wawili baada ya kuwakuta na hatia ya kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 15, wakimtuhumu kuiba alizeti katika shamba lao.

Waliohukumiwa ni Pieter Doorewaard (28) na Philip Schutte (35) ambao walimuua Matlhomola Mosweu.

Walidaiwa kutenda kosa hilo Aprili mwaka juzi. Jaji Ronald Hendricks alimhukumu Doorewaard kwenda jela miaka 18 na Schutte ni miaka 23.

Alisema ametoa hukumu hiyo badala ya kifungo cha maisha kwa kuwa ni kosa lao la kwanza. Mtoto huyo alivunjika shingo na kufariki dunia baada ya kurushwa kutoka kwenye gari lililokuwa likiendeshwa na washitakiwa hao.

Katika utetezi wao, wakulima hao walidai kwamba kijana huyo aliruka mwenyewe wakati wakiendesha gari kumpeleka polisi. Lakini ilibainika Schutte ndiye aliyemrusha mtoto huyo na kumsababishia kifo.

“Mlimchukua marehemu na kumrusha chini kutoka kwenye gari. Matendo mliyofanya yalikuwa ni aibu kabisa,” alisema.

Mashitaka dhidi ya matukio ya ubaguzi wa rangi baina ya wazungu wanaomiliki mashamba dhidi ya weusi yanatajwa kuwa mengi nchini hapa.

Mwaka 2016, wakulima wazungu, mashariki mwa jimbo la Mpumalanga walimlazimisha mtu mweusi kuingia kwenye jeneza wakimtuhumu kufanya makosa.

Baada ya tukio hilo kuoneshwa kwenye mitandao ya kijamii, wakulima hao walihukumiwa kwenda jela kati ya miaka 16 na 19.

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameongeza muda wa viza za ...

foto
Mwandishi: JOHANESBURG, Afrika Kusini

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi